Loading...

Mahakama kwenda Kidijitali

Loading...
Mahakama kwenda Kidijitali - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Mahakama kwenda Kidijitali, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Mahakama kwenda Kidijitali
link : Mahakama kwenda Kidijitali

soma pia


Mahakama kwenda Kidijitali

Na Mary Gwera, Mahakama

Mahakama ya Tanzania imedhamiria kufanya malipo yote ya huduma zake na ukusanyaji wa mapato kielektroniki ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya Teknolojia na vilevile kuboresha huduma kwa manufaa ya wananchi.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Msaidizi, Mipango na Bajeti-Mahakama ya Tanzania, Bw. Erasmus Uisso Januari 16, alipokuwa akifungua mafunzo ya Siku tano ya Mfumo wa Kielektroniki wa Kukusanya Mapato ya Serikali ‘Government Electronic Gateway (GEPG) yanayofanyika katika Ukumbi mpya ya Mikutano uliopo katika eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi-Kisutu jijini Dar es Salaam.

“Mahakama kama ilivyo kwa Taasisi nyingine za Serikali imejiunga katika Mfumo huu ili kufanya ukusanyaji wa Mapato na malipo yote ya Huduma za Mahakama kufanywa kwa njia ya Kieletroniki, kwa hiyo ili kuwezesha matumizi ya mfumo huu yameandaliwa mafunzo haya maalum kwa Watumiaji katika ngazi mbalimbali za Mahakama kuwapa ujuzi wa kuwawezesha kufanya kazi hii,” alifafanua Bw. Uisso.

Alitaja kuwa kwa kuanzia mafunzo hayo ya awamu ya kwanza yameshirikisha jumla ya Watumishi 35 wa Mahakama kwa Mkoa wa Dar es Salaam, akitaja watumishi hao kuwa ni pamoja na Wahasibu, Maafisa TEHAMA, Makarani kutoka Makao Makuu na ngazi zote za Mahakama kwa mkoa huu.

“Tunatarajia kuendelea kutoa elimu hiyo katika mikoa mingine kwa awamu, ili kuiwezesha Mahakama nchi nzima kutumia mfumo huu,” aliongeza Bw. Uisso.

 Afisa TEHAMA kutoka Wizara ya Fedha na Mipango-Kitengo cha Usimamizi wa Mifumo ya Fedha, Bi. Penina Henjewele akitoa Mada ya Mfumo wa Kielektroniki wa Kukusanya Mapato ya Serikali ‘Government Electronic Gateway (GEPG) kwa Washiriki wa Mafunzo hayo (hawapo pichani) 
 Mkurugenzi Msaidizi, Mipango na Bajeti-Mahakama ya Tanzania, Bw. Erasmus Uisso akiongea jambo na Washiriki katika mafunzo ya Siku tano ya Mfumo wa Kielektroniki wa Kukusanya Mapato ya Serikali ‘Government Electronic Gateway (GEPG) yanayofanyika katika Ukumbi mpya ya Mikutano uliopo katika eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi-Kisutu jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Sehemu ya Wahasibu na Makarani wa Mahakama wakiwa katika mafunzo ya Siku tano ya Mfumo wa Kielektroniki wa Kukusanya Mapato ya Serikali ‘Government Electronic Gateway (GEPG) yanayofanyika katika Ukumbi mpya ya Mikutano uliopo katika eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi-Kisutu jijini Dar es Salaam.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala Mahakama kwenda Kidijitali

yaani makala yote Mahakama kwenda Kidijitali Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Mahakama kwenda Kidijitali mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/mahakama-kwenda-kidijitali.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Mahakama kwenda Kidijitali"

Post a Comment

Loading...