Loading...

MWAKYEMBE ATEMBELEA KAMBI YA SERENGETI BOYS LEO JIJINI DAR

Loading...
MWAKYEMBE ATEMBELEA KAMBI YA SERENGETI BOYS LEO JIJINI DAR - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MWAKYEMBE ATEMBELEA KAMBI YA SERENGETI BOYS LEO JIJINI DAR, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MWAKYEMBE ATEMBELEA KAMBI YA SERENGETI BOYS LEO JIJINI DAR
link : MWAKYEMBE ATEMBELEA KAMBI YA SERENGETI BOYS LEO JIJINI DAR

soma pia


MWAKYEMBE ATEMBELEA KAMBI YA SERENGETI BOYS LEO JIJINI DAR

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Dr. Harrison Mwakyembe, Leo Jumamosi Januari 20, 2018 ameitembelea timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 16 Serengeti Boys iliyopo kambini kwenye hostel za Makao Makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF na kuwaachia ujumbe wa Serikali. 

Dr. Mwakyembe akitoa salamu za Serikali amewaambia Vijana wanaounda timu hiyo kuwa serikali inawaamini na wanalo jukumu la kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania. 

Amewataka kupambana kwa ajili ya Tanzania na kuhakikisha wanafanya vyema kwenye kila mashindano huku akiwataka makocha wa kikosi hicho kuwapa mafunzo mazuri kwa ustawi wa Vijana hao. 

Aidha Dr. Mwakyembe amesema anaamini Vijana hao watakuwa bora chini ya TFF iliyopo madarakani inayoongozwa na Rais Ndugu Wallace Karia. "Naamini mtaimarika na kuwa bora maana hata TFF hii sasa ina ari na morali kubwa".Alisema Dr. Mwakyembe. 

Katika ziara yake hiyo Dr. Mwakyembe alipata nafasi ya kutazama mchezo wa kirafiki kati ya Serengeti Boys na Makongo Sekondari iliyomalizika kwa Serengeti Boys kupata ushindi wa mabao 4-1.

Kabla ya mchezo huo Serengeti Boys walicheza mchezo mwingine wa kirafiki dhidi ya Kituo cha Bombom iliyomalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA TFF


Hivyo makala MWAKYEMBE ATEMBELEA KAMBI YA SERENGETI BOYS LEO JIJINI DAR

yaani makala yote MWAKYEMBE ATEMBELEA KAMBI YA SERENGETI BOYS LEO JIJINI DAR Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MWAKYEMBE ATEMBELEA KAMBI YA SERENGETI BOYS LEO JIJINI DAR mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/mwakyembe-atembelea-kambi-ya-serengeti.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MWAKYEMBE ATEMBELEA KAMBI YA SERENGETI BOYS LEO JIJINI DAR"

Post a Comment

Loading...