Loading...
title : NDOA ZA UTOTONI BADO NI TATIZO KUBWA TANZANIA NA AFRIKA MASHARIKI
link : NDOA ZA UTOTONI BADO NI TATIZO KUBWA TANZANIA NA AFRIKA MASHARIKI
NDOA ZA UTOTONI BADO NI TATIZO KUBWA TANZANIA NA AFRIKA MASHARIKI
Na,Jumbe Ismailly SINGIDA
TATIZO la ndoa za utotoni katika Tanzania na nchi za Afrika Mashariki limeonekana ni tatizo kubwa sana katika maeneo hayo ambapo kitakwimu inaonyesha kuwa kati ya mikoa kumi bora Mkoa wa Shinyanga unaongoza kwa kuwa na asilimia 59 na Mkoa wa Singida umeshika nafasi ya nane kwa kuwa na asilimia 42.
Meneja wa Shirika la kidini lisilokuwa la kiserikali la World Vision Tanzania (WVT) Kanda ya kati,Faraja kulanga aliyasema hayo kwenye uzinduzi wa mpango wa kutokomeza mimba za utotoni uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kanisa Katoliki,mjini Singida.
Alifafanua kwamba kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Tanzania Demokratic Health Survey ya mwaka 2010 inaonyesha kitakwimu kwamba tatizo la ndoa za utotoni,Mkoa unaoongoza ni Mkoa wa Shinyanga wenye asilimia 59 huku Mkoa wa Singida ukiwa na assilimia 42 na hivyo kushika nafasi ya nane katika mikoa hiyo kumi bora.
“Kwa maana kwamba ule utafiti huwa unakwenda kuuliza kila nyumba na wakiuliza katika kila nyumba mama alipata ujauzito katika umri gani,wale waliopata mimba katika umri chini ya miaka 18 ilikuwa ni asilimia 59.”alifafanua Kulanga.
Mkuu wa wilaya ya Singida,Eliasi Tarimo alipokuwa akizindua mpango wa mapambano dhidi ya ndoa za utotoni kwenye ukumbi wa Kanis Katoliki,mjini Singida.
baadhi ya wananchi waliohudhuria kwenye uzinduzi wa semina ya mapambano dhidi ya ndoa za utotoni uliofanyika katika ukumbi wa Kanisa Katoliki,mjini Singida.
baadhi ya wananchi waliohudhuria kwenye uzinduzi wa semina ya mapambano dhidi ya ndoa za utotoni uliofanyika katika ukumbi wa Kanisa Katoliki,mjini Singida.
Meneja wa World Vision Tanzania (WVT) Kanda ya kati,Faraja Kulangwa akiwasilisha mada juu ya madhumuni ya semina hiyo kwa wananchi waliohudhuria kwenye ukumbi wa mikutano wa Kanisa Katoliki,mjini Singida.
Hivyo makala NDOA ZA UTOTONI BADO NI TATIZO KUBWA TANZANIA NA AFRIKA MASHARIKI
yaani makala yote NDOA ZA UTOTONI BADO NI TATIZO KUBWA TANZANIA NA AFRIKA MASHARIKI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NDOA ZA UTOTONI BADO NI TATIZO KUBWA TANZANIA NA AFRIKA MASHARIKI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/ndoa-za-utotoni-bado-ni-tatizo-kubwa.html
0 Response to "NDOA ZA UTOTONI BADO NI TATIZO KUBWA TANZANIA NA AFRIKA MASHARIKI"
Post a Comment