Loading...
title : Nishati : Dkt. Kalemani akagua miradi ya uzalishaji Umeme Katavi
link : Nishati : Dkt. Kalemani akagua miradi ya uzalishaji Umeme Katavi
Nishati : Dkt. Kalemani akagua miradi ya uzalishaji Umeme Katavi
Na Teresia Mhagama, Katavi
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, amefanya ziara mkoani Katavi kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), mwaka 2017 ya kukamilisha ufungaji wa mitambo mipya ya kuzalisha umeme katika wilaya ya Mpanda na Mlele mkoani humo.
Dkt. Kalemani alitoa maagizo hayo baada ya mitambo iliyokuwepo katika kituo cha Mpanda kuharibika na hivyo kupelekea mkoa huo kuwa na changamoto ya upatikanaji wa umeme huku baadhi ya maeneo katika wilaya ya Mlele yakipata umeme kutoka nchini Zambia.
Meneja Miradi kutoka TANESCO, Stephen Manda alimweleza Dkt Kalemani kuwa, ufungaji wa mitambo ya umeme katika kituo cha Mpanda umekamilika na sasa kituo kinazalisha umeme wa kiasi cha megawati 2.5 huku matumizi ya wilaya ya Mpanda yakiwa ni megawati 2.3.
Manda alieleza kuwa, kukamilika kwa mitambo ya umeme katika kituo cha Mpanda kumewezesha vijiji 14 kusambaziwa umeme ikiwemo wilaya mpya ya Tanganyika ambayo imepata umeme kwa mara ya kwanza kutoka kuanzishwa kwake.
Akiwa katika wilaya ya Mlele, Dkt. Kalemani alielezwa kuwa, ufungaji wa mashine moja ya kuzalisha umeme yenye uwezo wa kilowati 476 umekamilika na kuwezesha baadhi ya wakazi wa Mlele hususan Makao Makuu ya wilaya hiyo (Inyonga) kupata umeme.
Baada ya kupata taarifa ya utekelezaji wa maagizo yake, Dkt Kalemani aliwapongeza wataalam wa TANESCO waliosimamia na kutekeleza kazi hiyo ndani ya wakati uliopangwa.
Aidha, alitoa maagizo kwa TANESCO ya kuongeza mitambo mingine miwili ya uzalishaji umeme katika kituo cha Mpanda na mmoja katika kituo cha Inyonga wilayani Mlele ili kuweza kuwa na umeme wa kutosha utakaowezesha wanannchi kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi ikiwemo uanzishaji wa Viwanda.
Kwa kuwa mitambo hiyo inatumia mafuta kuzalisha umeme, Dkt Kalemani alisema kuwa, Serikali ipo kwenye maandalizi ya kuanza ujenzi wa miundombinu ya kusafirisha umeme kwa msongo wa kV 400 kutoka mkoani Mbeya- Sumbawanga-Katavi - Kigoma hadi Nyakanazi. Hivyo mkoa wa Katavi utapata umeme wa gridi ya Taifa na kuachana na mitambo ya mafuta ambayo inatumia gharama kubwa.
Akizungumza na wananchi wilayani Mlele, Dkt Kalemani aliwaasa kujitokeza kwa wingi ili kuunganishwa na huduma ya umeme na hivyo kujiletea maendeleo huku akitolea mfano wilaya ya Mlele ambayo matumizi yake ya umeme ni kW 71 ambayo ni sawa na asilimia 15 tu ya uwezo wa mtambo.
Mkuu wa mkoa wa Katavi, Meja Jenerali (Mst), Raphael Muhuga alimshukuru Waziri wa Nishati kwa kutoa maagizo ya kufunga mashine nyingine tatu mpya za kufua katika mkoa wa Katavi suala ambalo litapelekea mkoa huo kuwa na umeme wa uhakika.
Vilevile aliisisitiza Wizara kuharakisha utekelezaji wa mradi wa umeme wa kilovolti 400 ambao kukamilika kwake kutafungua fursa za kiuchumi mkoani humo kutokana na kuwa na umeme wa kutosha na wa uhakika.
Katika ziara hiyo, Waziri Kalemani aliambatana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini, Dkt. Gidion Kaunda na Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO, Dkt. Alexander Kyaruzi ambao kwa nyakati tofauti waliwaasa wananchi kulinda miundombinu ya Umeme ili kutorudisha nyuma juhudi za Serikali za kusambaza umeme nchini.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani ( wa nne kulia) na Mkuu wa mkoa wa Katavi, Meja Jenerali (Mst), Raphael Muhuga (wa tano kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Wizara ya Nishati, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Katavi kabla ya kuanza ziara ya kukagua miradi ya kuzalisha umeme mkoani Katavi.
Meneja Miradi kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Makao Makuu, Stephen Manda (kulia), akitoa maelezo kuhusu mitambo ya uzalishaji umeme katika kituo cha Mpanda mkoani Katavi. Anayesikiliza ni Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani ( katikati) na Mkuu wa mkoa wa Katavi, Meja Jenerali (Mst), Raphael Muhuga (wa kwanza kushoto).
Mitambo ya umeme katika kituo cha Mpanda mkoani Katavi inayozalisha umeme wa kiasi cha megawati 2.5 kwa kutumia mafuta.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (kulia) akizungumza na wananchi wa Inyonge wilayani Mlele wakati alipofika wilayani humo kukagua mradi wa uzalishaji umeme.
Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO, Dkt Alexander Kyaruzi akizungumza na wananchi wa Inyonge wilayani Mlele wakati Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa pili kushoto) alipofika wilayani hapo kukagua mradi wa umeme. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Katavi, Meja Jenerali (Mst), Raphael Muhuga na Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mlele, Rachel Kasanda.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Dkt Gidion Kaunda akizungumza na wananchi wa Inyonge wilayani Mlele wakati Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa pili kushoto) alipofika wilayani hapo kukagua mradi wa umeme. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Katavi, Meja Jenerali (Mst), Raphael Muhuga na Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mlele, Rachel Kasanda.
Mtambo wa kuzalisha umeme katika kituo cha Inyonga, wilaya ya Mlele mkoani Katavi unaozalisha umeme wa kiasi cha kilowati 476 kwa kutumia mafuta.
Hivyo makala Nishati : Dkt. Kalemani akagua miradi ya uzalishaji Umeme Katavi
yaani makala yote Nishati : Dkt. Kalemani akagua miradi ya uzalishaji Umeme Katavi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Nishati : Dkt. Kalemani akagua miradi ya uzalishaji Umeme Katavi mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/nishati-dkt-kalemani-akagua-miradi-ya.html
0 Response to "Nishati : Dkt. Kalemani akagua miradi ya uzalishaji Umeme Katavi"
Post a Comment