Loading...

Profesa Mbarawa awataka TPA kukamilisha na kuhamia jengo jipya

Loading...
Profesa Mbarawa awataka TPA kukamilisha na kuhamia jengo jipya - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Profesa Mbarawa awataka TPA kukamilisha na kuhamia jengo jipya, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Profesa Mbarawa awataka TPA kukamilisha na kuhamia jengo jipya
link : Profesa Mbarawa awataka TPA kukamilisha na kuhamia jengo jipya

soma pia


Profesa Mbarawa awataka TPA kukamilisha na kuhamia jengo jipya

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameitaka Mamlaka ya Bandari nchini (TPA), kuhakikisha kazi ya kukamilisha ujenzi wa jengo jipya 'One Stop Centre' inakamilika haraka na kuanza kutoa huduma kwa mamlaka hiyo na wadau wake wote.

Akizungumza mara baada ya kukagua jengo hilo leo jijini Dar es Salaam, Prof. Mbarawa  amesema ufanisi wa bandari ya Dar es Salaam utafikiwa pale wadau wote wa bandari hiyo watakapofanya kazi saa 24 na katika eneo moja ili kumrahisishia mteja kupata huduma kwa haraka na katika kiwango kinachokubalika kimataifa.

"Natoa miezi sita kuanzia leo kwa TPA msimamieni mkandarasi  kikamilifu ili ikifika Juni muwe mmehamia ninyi na wadau wenu wote katika jengo hili," alisititiza Prof. Mbarawa katika ziara hiyo.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko amemhakikishia Prof. Mbarawa kuwa katika kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa wakati tayari yeye amehamia kwenye jengo hilo, ili kuongeza hamasa kwa mkandarasi kukamilisha ujenzi wake.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini (TPA), Eng. Deusdedit Kakoko (kulia)akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Mbarawa (kushoto) alipokagua jengo jipya 'One Stop Centre' la TPA leo.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (katikati) akitoa maelekezo katika ziara ya kukagua ujenzi wa jengo jipya 'One Stop Centre' la Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) lililopo bandarini leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini (TPA), Eng. Deusdedit Kakoko na Naibu Mkurugenzi wa TPA (Miundombinu), Eng. Karim Mattaka wakimsikiliza.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (katikati) akimsikiliza kwa makini mmoja wa abiria wa Kivuko cha Magogoni alipofanya ukaguzi wa kivuko hicho leo jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (katikati) akiwa na baadhi ya abiria wa Kivuko cha Magogoni mara baada ya ukaguzi wa kivuko hicho leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akisisitiza jambo katika ziara ya kukagua ujenzi wa jengo jipya 'One Stop Centre' la Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) lililopo bandarini leo jijini Dar es Salaam. 

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA



Hivyo makala Profesa Mbarawa awataka TPA kukamilisha na kuhamia jengo jipya

yaani makala yote Profesa Mbarawa awataka TPA kukamilisha na kuhamia jengo jipya Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Profesa Mbarawa awataka TPA kukamilisha na kuhamia jengo jipya mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/profesa-mbarawa-awataka-tpa-kukamilisha.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Profesa Mbarawa awataka TPA kukamilisha na kuhamia jengo jipya"

Post a Comment

Loading...