Loading...

RC TABORA: APONGEZA MATUMIZI YA NGUVU KAZI ZA JAMII (FORCE ACCOUNT) KATIKA UJENZI WA MABWENI YA ZIBA NA NANGA SEKONDARI.

Loading...
RC TABORA: APONGEZA MATUMIZI YA NGUVU KAZI ZA JAMII (FORCE ACCOUNT) KATIKA UJENZI WA MABWENI YA ZIBA NA NANGA SEKONDARI. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa RC TABORA: APONGEZA MATUMIZI YA NGUVU KAZI ZA JAMII (FORCE ACCOUNT) KATIKA UJENZI WA MABWENI YA ZIBA NA NANGA SEKONDARI., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : RC TABORA: APONGEZA MATUMIZI YA NGUVU KAZI ZA JAMII (FORCE ACCOUNT) KATIKA UJENZI WA MABWENI YA ZIBA NA NANGA SEKONDARI.
link : RC TABORA: APONGEZA MATUMIZI YA NGUVU KAZI ZA JAMII (FORCE ACCOUNT) KATIKA UJENZI WA MABWENI YA ZIBA NA NANGA SEKONDARI.

soma pia


RC TABORA: APONGEZA MATUMIZI YA NGUVU KAZI ZA JAMII (FORCE ACCOUNT) KATIKA UJENZI WA MABWENI YA ZIBA NA NANGA SEKONDARI.

NA TIGANYA VINCENT
RS TABORA
10 January 2018
SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imepongeza uongozi wa Shule za Sekondari za Nanga na Ziba wilayani Igunga kwa kusimamia vema ujenzi wa Mabweni ya wanafunzi wa shule hizo ambao unaotekezwa chini ya Mradi ya Lipa Kwa Matokeo (P4R) ambayo yamejengwa kwa kiwango cha juu na kwa gharama nafuu.
Kauli hiyo ilitolewa jana wilayani Igunga na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri baada ya kuzitembelea ili kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo ya mabweni hayo.
Alisema kuwa ujenzi huo ulitumia nguvu kazi ya jamii(force account) umesaidia kuwa na majengo mazuri ambayo yametumia fedha kidogo kuliko ambavyo wangetumia wakandarasi na kazi imemalizika mapema.
Mwanri alitoa ushauri kwa uongozi wa Shule hizo kuhakikisha wanaweka miundo mbinu ya maji hata kama maeneo hayo hajafikiwa na mfumo wa maji ya bomba ili itakapofika muda wasianze tena kuhangaika na mafundi hao.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka walimu hao kuhakikisha wanapanga barabara vizuri za Shule na kupanda miti na maua ili kuweka madhari ya shule yatakawavutia wanafunzi kujifunza na kupenda Shule.
Awali Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Ziba Pendo Ndaki alisema kuwa walipokea jumla ya shingi milioni 75 kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali ya Mitaa kwa ajili ya shughuli za ujenzi wa mabweni.
Alisema kuwa baada ya kuzipata na kukaa na Bodi ya Shule waliweza kumpata fundi na kufunga naye mkataba mwishoni mwa Oktoba mwaka jana na ndipo ujenzi ulianza na hadi sasa ameshakamilisha zaidi ya asilimia 60.
Ndaki aliongeza kuwa hadi hivi sasa kiasi cha shilingi milioni 32 zimetumika kununulia vifaa vya ujenzi na milioni 5.4 fundi zimelipwa kwa fundi na kubaki na milioni 37.5.
Alisema kuwa wanatarajia katikati ya mwezi huo bweni hilo lenye  uwezo wa kuchukua wanafunzi 80 watakaokuwa wakilala litakuwa limekamilika.
Kwa upande Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Nanga Steven Mzimya alisema kuwa shule yake ilifanikiwa kupokea shilingi milioni 241 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni na shughuli nyingine za ujenzi.
Alisema kuwa fedha hizo zimetumika katika ujenzi wa mabweni mawili yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 160, utengenezaji wa madawati 90, ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa na ujenzi wa matundu 10 ya vyoo.
Mzimya alisema kuwa shughuli zote ziko katika hatua za mwisho wakati wowote wanafunzi wataanza kuzitumia.
Ujenzi huo unatekelezwa chini ya Miradi ya Lipa Kwa Matokeo (P4R) ambapo kumekuwepo mafanikio mazuri katika shule mbalimbali mkoani Tabora


Hivyo makala RC TABORA: APONGEZA MATUMIZI YA NGUVU KAZI ZA JAMII (FORCE ACCOUNT) KATIKA UJENZI WA MABWENI YA ZIBA NA NANGA SEKONDARI.

yaani makala yote RC TABORA: APONGEZA MATUMIZI YA NGUVU KAZI ZA JAMII (FORCE ACCOUNT) KATIKA UJENZI WA MABWENI YA ZIBA NA NANGA SEKONDARI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala RC TABORA: APONGEZA MATUMIZI YA NGUVU KAZI ZA JAMII (FORCE ACCOUNT) KATIKA UJENZI WA MABWENI YA ZIBA NA NANGA SEKONDARI. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/rc-tabora-apongeza-matumizi-ya-nguvu.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "RC TABORA: APONGEZA MATUMIZI YA NGUVU KAZI ZA JAMII (FORCE ACCOUNT) KATIKA UJENZI WA MABWENI YA ZIBA NA NANGA SEKONDARI."

Post a Comment

Loading...