Loading...
title : SERIKALI KUPIMA MAENEO YAKE YOTE MWAKA HUU KUEPUSHA MIGOGORO NA WANANCHI
link : SERIKALI KUPIMA MAENEO YAKE YOTE MWAKA HUU KUEPUSHA MIGOGORO NA WANANCHI
SERIKALI KUPIMA MAENEO YAKE YOTE MWAKA HUU KUEPUSHA MIGOGORO NA WANANCHI
Na. Hassan Mabuye, Wizara ya Ardhi
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi amezitaka Wizara, Taasisi za Serikali na Vyombo vyote vya Umma kupima maeneo yao na kuyawekea alama za mipaka ili kuepusha maeneo hayo kuvamiwa na wananchi.
Waziri Lukuvi amesema hayo mara baada ya kukagua maeneo yaliyo na migogoro ya ardhi katika manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza.
Aidha Mheshimiwa Lukuvi akiambata na Naibu wake ambaye ni mbunge wa Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza walitembelea maeneo yaliyovamiwa na wananchi ya Polisi Kigoto-Kirumba lililovamiwa na wananchi, Uwanja wa Ndege wa Mwanza na eneo la Jeshi la Wananchi wa Tanzania la Nyamirolerwa katika manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza.
Kutokana na kujionea uvamizi huo wa maeneo hayo, Waziri Lukuvi amezitaka taazizi zote za serikali kupima maeneo yao ili wananchi waweze kutambua maeneo ya Serikali wasiweze kuyavamia jambo ambalo huzaa migogoro.
Hata hivyo Waziri Lukuvi amewataka wananchi waliojenga ndani ya hifadhi ya Uwanja wa Ndege wa Mwanza kuondoa maendelezo yao ndani ya siku saba kabla kuchukuliwa hatua kwakuwa ni wavamizi na hawaruhusiwi kukaa karibu na eneo linalorusha na kutua vyombo vya anga jambo ambalo ni hatari kwao na usalama wa vyombo hivyo.
"Hawa waliojenga ni wavamizi na watambue hivyo majibu tutatoa badaye nini tutafanya lakini wajue maisha yao siyo ya hapo ndani ya uwanja," alisema lukuvi.Na katika hatua nyingine Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya makazi William Lukuvi amezitaka halmashauri zote nchini kukamilisha zoezi la ukusanyaji wa kodi ya Ardhi kabla ya tarehe 30 mwezi Aprili mwaka huu.
Hivyo makala SERIKALI KUPIMA MAENEO YAKE YOTE MWAKA HUU KUEPUSHA MIGOGORO NA WANANCHI
yaani makala yote SERIKALI KUPIMA MAENEO YAKE YOTE MWAKA HUU KUEPUSHA MIGOGORO NA WANANCHI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI KUPIMA MAENEO YAKE YOTE MWAKA HUU KUEPUSHA MIGOGORO NA WANANCHI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/serikali-kupima-maeneo-yake-yote-mwaka.html
0 Response to "SERIKALI KUPIMA MAENEO YAKE YOTE MWAKA HUU KUEPUSHA MIGOGORO NA WANANCHI"
Post a Comment