Loading...
title : SHERIA YA TAKWIMU MWAKA 2015 HAIJAZUIA TAFITI ELIMU YA JUU
link : SHERIA YA TAKWIMU MWAKA 2015 HAIJAZUIA TAFITI ELIMU YA JUU
SHERIA YA TAKWIMU MWAKA 2015 HAIJAZUIA TAFITI ELIMU YA JUU
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
MKURUGENZI wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dk.Albina Chuwa amesema sheria ya Takwimu ya mwaka 2015, hazigusi tafiti zinazofanywa na Vyuo Vikuu nchini kutokana na taratibu wanazozifanya zinakidhi maadili ya kufanya tafiti hizo katika masomo mbalimbali ya wanafunzi wa elimu ya juu.
Amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anafungua mkutano wa uelimishaji umma kuhusu Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015 na kueleza NBS haijazuia vyuo kufanya tafiti zake katika masomo.Dk.Chuwa ameongeza sheria hiyo imekuwa ikileta changamoto kwa baadhi ya taasisi vikiwemo vyuo vikuu katika uandaji wa tafiti za kimasomo kwa wanafunzi.
Dk.Chuwa amesema sheria ya takwimu ya mwaka 2015 haijazuia mtu au taasisi yoyote kutoa takwimu badala yake sheria hiyo imetoa wigo na kuweka misingi ya njia bora zinazotakiwa kufuatwa na wadau wa takwimu katika mchakato wa uzalishaji takwimu rasimi.
Amefafanua NBS haiwezi kutoa takwimu rasmi yenyewe bila kushirikiana na wadau ambao ndio watumiaji katika kuharakisha maendeleo ya nchi."Takwimu rasmi zina kanuni na miongozo yake ya kutumia hadi kutumika kupanga sera bora za kuleta maendeleo kwa wananchi,"amesema Dk.Chuwa.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dk.Albina Chuwa akizungumza wakati akifungua mkutano wa wadau kuhusiana na Uelimishaji Umma kuhusu Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015, leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Waratibu wa Jukwaa la Maendeleo Endelevu –Tanzania, Stephen Chacha akizungumza katika mkutano kuhusu namna ya kushirikiana na NBS leo jijjini Dar es Salaam.
Mwanasheria wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Oscar Mangula akizungumza katika mkutano wa wadau kuhusiana na sheria ya Taifa ya Takwimu leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau katika mkutano wa wadau wa Takwimu
Hivyo makala SHERIA YA TAKWIMU MWAKA 2015 HAIJAZUIA TAFITI ELIMU YA JUU
yaani makala yote SHERIA YA TAKWIMU MWAKA 2015 HAIJAZUIA TAFITI ELIMU YA JUU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SHERIA YA TAKWIMU MWAKA 2015 HAIJAZUIA TAFITI ELIMU YA JUU mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/sheria-ya-takwimu-mwaka-2015-haijazuia.html
0 Response to "SHERIA YA TAKWIMU MWAKA 2015 HAIJAZUIA TAFITI ELIMU YA JUU"
Post a Comment