Loading...
title : STAMICO WATAKIWA KUTATHIMINI UTENDAJI WAO-Biteko
link : STAMICO WATAKIWA KUTATHIMINI UTENDAJI WAO-Biteko
STAMICO WATAKIWA KUTATHIMINI UTENDAJI WAO-Biteko
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
NAIBU Waziri wa Madini, Dotto Biteko amelitaka Shirika la Taifa la Madini (Stamico) kujitathini kuhusu utendaji wao wa kazi kwa Taifa kutokana na kuwa deni kubwa kuliko uzalishaji wa shirika hilo.
Biteko ametoa kauli hiyo alipotembelea Shirika la Taifa la Madini (Stamico) leo, Dar es Salaam,ambapo amesema Stamico imekuwa na madeni yanayofanya kudidimiza shirika kutokana na miradi wanayoiendesha ya uchimbaji kushindwa kuzalisha faida.
Amesema baada ya watu kujua changamoto sasa ndio wameona sehemu kujengea hoja katika taarifa mbalimbali.Biteko amesema Stamico ilitakiwa kuwa sehemu ya kujifunzia kwa wachimbaji wadogo lakini wachimbaji wadogo hawawezi kufika Stamico kwa sababu hakuna cha kujifunza.
Stamico inadeni zaidi ya Sh.bilioni moja pamoja na deni la Stamigold la Sh.bilioni 54 na Serikali inatakiwa kulipa deni hilo na kuacha kununua madawati katika shule.Biteko amesema kuwa kunahitajika kuwepo ubunifu kwa Stamico kwa kujiona wana kazi ya ziada ya kusaidia Taifa kupiga hatua.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Stamico, Alex Rutagwelela amesema kuwa maagizo watayafanyia kazi katika uendeshaji wa shirika hilo.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko akisitiza jambo wakati akizungumza na Uongozi pamoja na watumishi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Mtaa wa Upanga Jijini Dar es salaam, Leo 16 Januari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko akikagua mtambo wa uchongaji mashimo kwa ajili ya utafiti wakati alipotembelea Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Mtaa wa Upanga Jijini Dar es salaam, Leo 16 Januari 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko akisitiza wakati wa kikao cha pamoja na Uongozi pamoja na watumishi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Mtaa wa Upanga Jijini Dar es salaam, Leo 16 Januari 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko akisitiza wakati wa kikao cha pamoja na Uongozi pamoja na watumishi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Mtaa wa Upanga Jijini Dar es salaam, Leo 16 Januari 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Mtaa wa Upanga Jijini Dar es salaam, Leo 16 Januari 2018.
Hivyo makala STAMICO WATAKIWA KUTATHIMINI UTENDAJI WAO-Biteko
yaani makala yote STAMICO WATAKIWA KUTATHIMINI UTENDAJI WAO-Biteko Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala STAMICO WATAKIWA KUTATHIMINI UTENDAJI WAO-Biteko mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/stamico-watakiwa-kutathimini-utendaji.html
0 Response to "STAMICO WATAKIWA KUTATHIMINI UTENDAJI WAO-Biteko"
Post a Comment