Loading...
title : TIMU YA USIMAMIZI WA HUDUMA YA AFYA WILAYA YA LINDI YAAGIZWA KUSIMAMIA UKARABATI WA VITUO VYA AFYA
link : TIMU YA USIMAMIZI WA HUDUMA YA AFYA WILAYA YA LINDI YAAGIZWA KUSIMAMIA UKARABATI WA VITUO VYA AFYA
TIMU YA USIMAMIZI WA HUDUMA YA AFYA WILAYA YA LINDI YAAGIZWA KUSIMAMIA UKARABATI WA VITUO VYA AFYA
Angela Msimbira- OR-TAMISEMI LINDI.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bw. Ganchwele Makenge ameiagiza timu ya usimamizi wa huduma ya afya Wilaya ya Lindi kuhakikisha wanasimamia na kufuatilia ukarabati wa vituo vya afya ili vijengwe kwa ubora unaotakiwa kulingana na thamani ya fedha zilizotolewa na Serikali.
Ameyasema hayo kwenye kikao cha pamoja kati ya wataalam kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) kwa kushiriana na wataalam kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Halmashauri ya Lindi mara baada ya kukagua ujenzi wa kituo cha afya cha Nyangamara kilichopo kata ya Nyangamara, Wilaya ya Lindi Mkoani Lindi.
Bw. Makenge amesema Kamati ya Usimamizi wa Huduma ya Afya inalojukumu kubwa la kusimamia shughuli zote za afya katika Mkoa wa Lindi hivyo hawana budi kuhakikisha Miradi inayotekelezwa na Serikali inasimamiwa kikamilifu ikiwepo Ya ukarabati wa vituo vya afya nchini.
Amesema kuwa Kamati hiyo inahitajika kusimamia wahudumu wa afya katika kuhakikisha wanafanya kazi kwa kufuata kanuni taratibu na sheria za utumishi wa umma kwa kuwahudumia wananchi ipasavyo na kuondoa malalamiko yaliyopo katika sekta ya afya.
Ameiagiza kamati hiyo kusimamia utendaji bora katika vituo vya afya vya Mkoa wa Lindi kwa kuwahimiza wafanyakazi kutumia lugha nzuri kwa wagonjwa na kutoa huduma stahiki kwa jamii ili kuondoa kero mbalimbali ambazo wananchi wamekuwa wakizituhumu katika sekta ya afya nchini.
Baadhi ya Wataalam kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) pamoja na wataalam kutoka Mkoa wa Lindi wakikagua Ujenzi wa jengo la maabara lililojengwa katika kituo cha afya cha Nyangamara Mkoani Lindi.
Mwonekano wa Nyumba ya Mtumishi iliyojengwa katika kituo cha afya cha Nyangamara kilichopo katika Kata ya Nyamara, wilaya ya Lindi Mkoa wa Lindi.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala TIMU YA USIMAMIZI WA HUDUMA YA AFYA WILAYA YA LINDI YAAGIZWA KUSIMAMIA UKARABATI WA VITUO VYA AFYA
yaani makala yote TIMU YA USIMAMIZI WA HUDUMA YA AFYA WILAYA YA LINDI YAAGIZWA KUSIMAMIA UKARABATI WA VITUO VYA AFYA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TIMU YA USIMAMIZI WA HUDUMA YA AFYA WILAYA YA LINDI YAAGIZWA KUSIMAMIA UKARABATI WA VITUO VYA AFYA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/timu-ya-usimamizi-wa-huduma-ya-afya.html
0 Response to "TIMU YA USIMAMIZI WA HUDUMA YA AFYA WILAYA YA LINDI YAAGIZWA KUSIMAMIA UKARABATI WA VITUO VYA AFYA"
Post a Comment