Loading...
title : TRA INATARAJIA KUSAJILI WAFANYABIASHARA WADOGO MILIONI MOJA NCHI NZIMA
link : TRA INATARAJIA KUSAJILI WAFANYABIASHARA WADOGO MILIONI MOJA NCHI NZIMA
TRA INATARAJIA KUSAJILI WAFANYABIASHARA WADOGO MILIONI MOJA NCHI NZIMA
Na Chalila Kibuda, Globu
Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) imesema kuwa wanatarajia kusajili walipakodi wapya milioni moja (1,000,000) ambao watalipa kodi ya shilingi Bilioni 1.5.
Kodi zinazolipwa ndizo zinafanya serikali kutoa huduma bora kwa wananchi ikiwemo miundombinu ya barabara, afya, maji na huduma nyinginezo.
Akizungumza katika usajili wa kituo cha kusajili wafanyabiashara wadogo wadogo cha Chanika, Kamishna wa Kodi za Ndani, Elijah Mwandumbya amesema kuwa kampeni ya kusajili wafanyabiashara wa dogo ni endelevu.
Elijah amesema kuwa wananchi Wajitokeze kusajiliwa kadri kodi zinavyolipwa ndiyo zinafanya maendeleo ya nchi.
Amesema kuwa uhamasishaji wa ulipaji kodi na usajili utaendelea kwa kuweka vituo karibu na wafanyabiashara hao.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka hiyo, Richard Kayombo amewataka wananchi wa naoishi maeneo hayo kujitokeza kwa wingi kwaajili ya kujiandikisha na kusema kuwa zoezi hilo katika Kituo hicho Litadumu kwa muda wa juma moja.
Kayombo amesema wakitoka Manispaa ya Ilala watakwenda Manispaa ya Temeke na baadaye kufungua vituo katika maeneo mbalimbali" alisema Kayombo.
Aidha Kayombo amesema, Mamlaka hiyo imeamua kuja na kampeni hii baada ya kutambua kuwa kulikuwa na usumbufu kwa Wafanyabiashara kupata TIN namba, kutokana na umbali kutoka wakazi wa eneo hilo hadi Vingunguti, na sasa wamesomea huduma hiyo na kwamba watakaojiandikisha hawana ulazima kulipa kodi siku hiyo hiyo.
Pamoja na hayo amewatahadhalisha wananchi kutolaghaiwa na matapeli kwani kazi hiyo inafanywa na TRA yenyewe na hakuna wakala aliye pewa kazi hiyo.
Kamishna wa Kodi za Ndani, Elijah Mwandumbya akizungumza na waandishi habari juu ya usajili wa wafanyabiashara wadogo katika kituo cha Chanika jijini Dar es Salaam.
Mfanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Regina Urio (kulia) akimhudumia mfanyabiashara (kushoto) aliyefika katika kituo maalum kilichoteuliwa na mamlaka hiyo kilichopo Chanika jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusajili na kupata Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN).
Hivyo makala TRA INATARAJIA KUSAJILI WAFANYABIASHARA WADOGO MILIONI MOJA NCHI NZIMA
yaani makala yote TRA INATARAJIA KUSAJILI WAFANYABIASHARA WADOGO MILIONI MOJA NCHI NZIMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TRA INATARAJIA KUSAJILI WAFANYABIASHARA WADOGO MILIONI MOJA NCHI NZIMA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/tra-inatarajia-kusajili-wafanyabiashara.html
0 Response to "TRA INATARAJIA KUSAJILI WAFANYABIASHARA WADOGO MILIONI MOJA NCHI NZIMA"
Post a Comment