Loading...

TRA YAJIZATITI KUONGEZA IDADI YA WALIPAKODI

Loading...
TRA YAJIZATITI KUONGEZA IDADI YA WALIPAKODI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TRA YAJIZATITI KUONGEZA IDADI YA WALIPAKODI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TRA YAJIZATITI KUONGEZA IDADI YA WALIPAKODI
link : TRA YAJIZATITI KUONGEZA IDADI YA WALIPAKODI

soma pia


TRA YAJIZATITI KUONGEZA IDADI YA WALIPAKODI




Na: Veronica Kazimoto, 04 Januari, 2018, 
Dar es Salaam. 

Mwaka huu wa fedha wa 2017/18, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imedhamiria kuongeza idadi ya walipakodi kwa ajili ya kuisaidia nchi yetu kupunguza kutegemea misaada kutoka kwa wahisani. 

Lengo kuu la kuongeza walipakodi ni kupanua wigo na kuongeza makusanyo ambayo hutumika katika kuleta maendeleo na kujenga uchumi wa nchi. 

TRA ina mikakati mbalimbali ambayo imechukuliwa na inaendelea kutekelezwa ili kuhakikisha kuwa, walipakodi wanaongezeka na hatimaye kuongeza mapato ya Serikali. 

Mikakati hiyo ni pamoja na kusajili walipakodi ambapo Mamlaka imezindua kampeni ya usajili wa walipakodi nchi nzima ili kuhakikisha kwamba kila mfanyabiashara anasajiliwa na kupata Namba ya Utambulisho ya Mlipakodi (TIN) kwa urahisi na haraka. 

Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni, Kamishna wa Kodi za Ndani Elijah Mwandumbya wa Mamlaka ya Mapato Tanzania alisema, usajili wa walipakodi ni chanzo cha kuongeza idadi ya walipakodi na mapato kwa ujumla. 

"Moja ya majukumu ya msingi ya TRA ni Usajili wa Walipakodi ambao huongeza idadi ya walipakodi, wigo wa ulipaji kodi, makusanyo pamoja na kutoa taarifa sahihi za walipakodi wanaostahili kukadiriwa na kutozwa kodi ili kuchangia Pato la Taifa", Alisema Mwandumbya. 

Mwandumbya alisisitiza kuwa, walipakodi wadogo wanaostahili kulipa kodi kwa njia ya makadirio, watalipa robo ya kwanza ndani ya siku tisini (90) kuanzia waliposajiliwa tofauti na utaratibu uliokuwepo kwa kulipa kodi hiyo hata kabla mfanyabishara hajaanza kufanya biashara husika. 

"Wananchi wanaostahili kusajiliwa kama walipakodi ni watu wote wanaotarajia kuanzisha biashara, kumiliki vyombo vya usafiri kama vile gari na pikipiki, wanaostahili kulipa kodi ya majengo, wanaoingiza bidhaa kutoka nje ya nchi na wanaotarajia kupata leseni za udereva", alifafanua Mwandumbya. 



Hivyo makala TRA YAJIZATITI KUONGEZA IDADI YA WALIPAKODI

yaani makala yote TRA YAJIZATITI KUONGEZA IDADI YA WALIPAKODI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TRA YAJIZATITI KUONGEZA IDADI YA WALIPAKODI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/tra-yajizatiti-kuongeza-idadi-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TRA YAJIZATITI KUONGEZA IDADI YA WALIPAKODI"

Post a Comment

Loading...