Loading...
title : UCHAGUZI WA BFT KUFANYIKA TAREHE 24 MWEZI FEBRUARI MWAKA HUUA
link : UCHAGUZI WA BFT KUFANYIKA TAREHE 24 MWEZI FEBRUARI MWAKA HUUA
UCHAGUZI WA BFT KUFANYIKA TAREHE 24 MWEZI FEBRUARI MWAKA HUUA
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
BARAZA la Michezo la Taifa (BMT) limetangaza uchaguzi wa Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT) unaotarajiwa kufanyika tarehe 24 mwezi februari mwaka huu.
Akizungumzia kuanza kwa uchukuaji wa fomu hizo leo Jumatano Januari 17, Afisa habari wa BMT, Najaha Bakari amesema kuwa uchaguzi huo utafanyika Mkoani Dodoma na mwisho wa kuchukua fomu utakuwa ni Februari 15.
Najaha amesema kuwa, nafasi zinazogombaniwa ni nafasi ya rais,makamu wa rais, katibu mkuu, Mweka hazina na Wajumbe 9 watakaochaguliwa katika uchaguzi mkuu.
"Uchaguzi utakuwa ni katika nafasi za rais,makamu wa rais, katibu mkuu,mweka hazina na wajumbe 9 watakaochaguliwa kwenye uchaguzi mkuu ambapo kabla ya kuingia katika uchaguzi watapita kwenye usajili,"amesema Najaha.
Najaha ametaja vigezo vya wagombea hao katika nafasi mbalimbali ni kuwa mgombea haruhusiwi kugombea nafasi yoyote kama yeye ni mchezaji wa mchezo huo, mgombea awe na umri usiopungua miaka 25, asiwe ametenda kosa lolote la jinai, elimu kuanzia kidato cha nne na kuendelea.
Kwenye nafasi ya mweka hazina mgombea lazima awe na cheti cha uhasibu pia wajumbe wanaogombea nafasi hiyo lazima wawe na uzoefu na ngumi za ridhaa.
Kwa upande wa Rais wa Shirikisho la Ngumi BFT Mwita Rwakatare amesema kuwa ana imani uchaguzi huo utakaofanyika Februari 24 utakuwa wa amani pia amewasihi wadau wa mchezo wa ngumi kujitokeza kwa wingi kuja kuchukua fomu zitakazokuwa zinapatikana ofisi za BMT na BFT huku wagombea wote watachukua fomu na kulipia kupitia akaunti ya benki ya BMT.
Rais wa Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT) Mwita Rwakatare akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uchaguzi wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika Februari 24 mwaka huu Mkoani Dodoma.
Afisa wa Habari wa Baraza la Michezo la Taifa ( BMT) Najaha Bakari akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam.
Hivyo makala UCHAGUZI WA BFT KUFANYIKA TAREHE 24 MWEZI FEBRUARI MWAKA HUUA
yaani makala yote UCHAGUZI WA BFT KUFANYIKA TAREHE 24 MWEZI FEBRUARI MWAKA HUUA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UCHAGUZI WA BFT KUFANYIKA TAREHE 24 MWEZI FEBRUARI MWAKA HUUA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/uchaguzi-wa-bft-kufanyika-tarehe-24.html
0 Response to "UCHAGUZI WA BFT KUFANYIKA TAREHE 24 MWEZI FEBRUARI MWAKA HUUA"
Post a Comment