Loading...
title : WAANDISHI WA HABARI KORTINI KWA KUJIFANYA MAAFISA WA USALAMA.
link : WAANDISHI WA HABARI KORTINI KWA KUJIFANYA MAAFISA WA USALAMA.
WAANDISHI WA HABARI KORTINI KWA KUJIFANYA MAAFISA WA USALAMA.
Waandishi wa habari watano wilayani Kahama mkoani Shinyanga wamefikishwa mahakamani wilayani Kahama kwa makosa ya kujifanya maafisa usalama wa taifa na kujipatia fedha shilingi Milioni 1 kutoka kwa mganga wa jadi.
Waandishi hao wa habari ambao ni Paul Kayanda wa gazeti la Uhuru,Raymond Mihayo- Habarileo,Shaban Njia – Jamboleo,Simon Dioniz – Radio Kwizera na George Maziku ambaye hajulikani anaandikia chombo gani wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Kahama leo Jumatano Januari 10,2018.
Waandishi hao walikamatwa jana saa saba na nusu mchana na jeshi la polisi wakijifanya maafisa wa usalama wa taifa kutoka Dar es salaam,Kigoma,Kagera,Shinyanga na Kahama kisha kujipatia shilingi 1,000,000/- kutoka kwa mganga wa jadi Jane Mbeshi (46) mkazi wa kitongoji cha Ng’wande kata ya Mwaluguli wilayani Kahama baada ya kumtishia kuwa anapiga ramli chonganishi.
Walikamatwa baada ya kuwekewa mtego kwani waliahidiwa fedha zingine tena shilingi milioni 1 na mganga huyo wa jadi baada ya kuchukua shilingi milioni 1 tarehe 6.1.2018.
Waandishi hao wa habari Shaban Njia,Paul Kayanda,Simon Dioniz na Raymond Mihayo wamepelekwa gerezani baada kushindwa kutimiza masharti ya dhamana huku George Maziku akiendelea kutafutwa kwani bado hajapatikana,alishiriki kuchukua fedha 6.1.2018,jana hakukuenda kuchuchua fedha.
Hivyo makala WAANDISHI WA HABARI KORTINI KWA KUJIFANYA MAAFISA WA USALAMA.
yaani makala yote WAANDISHI WA HABARI KORTINI KWA KUJIFANYA MAAFISA WA USALAMA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAANDISHI WA HABARI KORTINI KWA KUJIFANYA MAAFISA WA USALAMA. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/waandishi-wa-habari-kortini-kwa.html
0 Response to "WAANDISHI WA HABARI KORTINI KWA KUJIFANYA MAAFISA WA USALAMA."
Post a Comment