Loading...
title : WAMILIKI NYUMBA 59 KIPUNGUNI A WAPEWA SIKU SABA WAHAME
link : WAMILIKI NYUMBA 59 KIPUNGUNI A WAPEWA SIKU SABA WAHAME
WAMILIKI NYUMBA 59 KIPUNGUNI A WAPEWA SIKU SABA WAHAME
JOPO la maofisa wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA), limefanya utambuzi wa nyumba 59 zilizopo eneo la Kipunguni A, jijini Dar es Salaam na kutoa notisi ya siku saba kwa wakazi wake kuhama.Nyumba hizo ni zile ambazo serikali tayari ililipa wakazi wake stahiki zao mwaka 2014 kufuatia uthamini uliofanyika mwaka 1997, lakini bado wanachi hao waliendelea kuishi eneo hilo linalohitajika na Serikali kwa ajili ya matumizi ya shughuli za Mamlaka ya Viwanja vya N dege.
Akizungumza baada ya kukamilika kwa shughuli hiyo ya utambuzi iliyofanyika leo Januari 25, Ofisa Ardhi mkuu wa TAA, Cecilia Mwing'uri amesema jopo hilo lilijumuisha watumishi kutoka TANESCO, Polisi, TAA kitengo cha sharia na Mahusiano, na wajumbe wa eneo hilo waliowawakilisha wananchi.
"Tulizitambua nyumba husika na kuziwekea alama ya X na kutoa notisi ili wakazi ambao bado wapo eneo hilo la Kipunguni wahame ndani ya siku saba kuanzia leo."Kwa bahati nzuri kuna ambao wamehama na wengine wanaendelea na ubomoaji wa kistaarabu wa nyumba zao isipokuwa wachache ambao waliuziwa nyumba na maeneo huku wamiliki wa kwanza wakijua fika, eneo hilo ni mali ya serikali na walishalipwa fedha zao," amesema.
Kwenye zoezi hilo Bi Cecilia alisema watumishi wa Shirika la Umeme (TANESCO), kutoka mkoa wa kihuduma wa Gongo la Mboto walitoa siku tatu kuanzia kesho na kwamba baada ya hapo wataanza zoezi la kuondoa miundombinu ya umeme kwenye nyumba husika ili kurahisisha zoezi la ubomoaji.
Mwishoni mwa mwaka jana, wakati wa ziara ya Naibu waziri wa mawasiliano na uchukuzi Mhandisi Atashasta Nditiye kwenye makao makuu ya TAA, alikutana na hoja hiyo na kuagiza Mamlaka hiyo ya Viwanja vya Ndege kuhakikisha waliolipwa fidia na bado wapo Kipunguni A wanaondoka ndani ya siku 30.
Amesema kwa kuwa serikali tayari imekamilisha jukumu lake kwa nafasi yake, hakuna budi watu hao wakahama ili nia ya serikali kwenye eneo hilo kama ni upanuzi wa kiwanja cha ndege au shughuli nyingine itekelezwe kwa nafasi.
Katika mazungumzo yake na watumishi wa TAA akiwemo Mkurugenzi Mkuu, Richard Mayongela, Mhandisi Nditiye aliahidiwa kuwa mamlaka hiyo itahakikisha wakazi ambao tayari wamelipwa fidia katika awamu iliyohusisha nyumba 59 inatekelezwa, kama ambavyo TAA imeanza kufanya leo.
Mhandisi Astelius John kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania akitoka kuweka alama ya kuondolewa kwa moja ya nyumba zilizolipwa fidia eneo la Kipunguni A.
Moja ya Nyumba zilizoanza kubomolewa na mwananchi mwenyewe katika eneo la Kipunguni A.
Afisa ardhi Mkuu kutoka Mamlaka ya viwanja Vya Ndege Bi Cecilia Mwing’uri akisaidia zoezi la kuweka alama ya kuondoa nyumba hiyo kati ya nyumba 59 zinazotakiwa kubomolewa.
Hivyo makala WAMILIKI NYUMBA 59 KIPUNGUNI A WAPEWA SIKU SABA WAHAME
yaani makala yote WAMILIKI NYUMBA 59 KIPUNGUNI A WAPEWA SIKU SABA WAHAME Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAMILIKI NYUMBA 59 KIPUNGUNI A WAPEWA SIKU SABA WAHAME mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/wamiliki-nyumba-59-kipunguni-wapewa.html
0 Response to "WAMILIKI NYUMBA 59 KIPUNGUNI A WAPEWA SIKU SABA WAHAME"
Post a Comment