Loading...
title : WANAKILOSA WATAKIWA KUHIFADHI MAZINGIRA KUEPUKA MAFURIKO
link : WANAKILOSA WATAKIWA KUHIFADHI MAZINGIRA KUEPUKA MAFURIKO
WANAKILOSA WATAKIWA KUHIFADHI MAZINGIRA KUEPUKA MAFURIKO
Kufuatia mafuriko yaliyotokea tarehe 11 hadi 19 Januari mwaka huu wilayani Kilosa na kusababisha athari kwa nyumba 384 kubomoka, nyumba 2,216 kuingiliwa na maji, Kaya 2,542 zenye watu 9,479 kuathirika. Baraza la maafa la wilaya hiyo limebainisha moja ya sababu kubwa ya mafuriko hayo ni uharibifu wa Mazingira.
Akiongea mara baada ya kutembelea maeneo yaliyoathirika na maafa ya mafuriko wilayani Kilosa, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa Faustin Kamuzora, alibainisha kuwa baada ya kujionea athari hizo na kuwasilishwa kwa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za maafa wilayani humo ambayo ilibainisha sababu tano za kutokea mafuriko wilayani humo, sababu hizo zote zimeonekana msingi wake ni uharibifu wa Mazingira.
“Nimeelezwa hapa Shughuli za kibinadamu ikiwa ni pamoja na makazi, Kilimo kando kando ya mto mkondoa zimechangia mafuriko, pia mto Mkondoa kubadilisha uelekeo na kubomoa tuta, lakini pia kujaa mchanga katika mto na kupunguza kina cha maji pamoja na bwawa la Kidete lilokuwa likitumika kuhifadhi na kupunguza kasi ya maji ya mto mkondoa kuharibika, niwasihi wanakilosa wahifadhi mazingira kuepuka haya” Alisema Kamuzora.
Kamuzora aliongeza kuwa Halmashauri hiyo haina budi kuzingatia sheria za maafa na mazingira kwa kuwaelimisha wanakilosa umuhimu wa kuhifadhi mazingira. Aidha aliishauri halmashauri hiyo kuandaa mfumo wa tahadhari za awali utakao wawezesha wananchi hao kuweza kupata taarifa za awali za mvua kunyesha kutoka katika maeneo ya jirani ili waweze kujiandaa na kukabili maafa ya mafuriko.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa Faustin Kamuzora akifafanua kwa baadhi ya wajumbe wa Baraza la maafa wilayani Kilosa, umuhimu wa kuhifadhi mazingira kama njia ya kuepuka maafa, wakati alipotembelea maeneo yaliyoathirika na maafa ya mafuriko wilayani humo yaliyotokea tarehe 11 hadi 19 Januari mwaka huu.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa Faustin Kamuzora (katikati) akiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Kilosa, Adamu Mgoyi kutembelea makazi hatarishi ya maafa ya mafuriko ambayo wakazi wa maeneo hayo wameamuliwa kuhama kwa Amri halali Na KLS/03/208 ya Mkuu wa wilaya hiyo na kugawiwa viwanja 1204 kwenye makazi mapya na salama.
Muonekano wa Sehemu ya Reli ya kati wilayani Kilosa ilivyoathirika na maafa ya mafuriko yaliyotokea tarehe 11 hadi 19 Januari mwaka huu, baada ya mto mkondoa kubomoa tuta na kubadili mwelekeo na kumega sehemu ya ardhi ya reli hiyo.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU).
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WANAKILOSA WATAKIWA KUHIFADHI MAZINGIRA KUEPUKA MAFURIKO
yaani makala yote WANAKILOSA WATAKIWA KUHIFADHI MAZINGIRA KUEPUKA MAFURIKO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WANAKILOSA WATAKIWA KUHIFADHI MAZINGIRA KUEPUKA MAFURIKO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/wanakilosa-watakiwa-kuhifadhi-mazingira.html
0 Response to "WANAKILOSA WATAKIWA KUHIFADHI MAZINGIRA KUEPUKA MAFURIKO"
Post a Comment