Loading...

WANANCHI WILAYA YA CHEMBA WAHAMASISHWA KUTUMIA FURSA YA KUJIPATIA KIPATO KWA KUTUMIA MIFUGO WALIYONAYO

Loading...
WANANCHI WILAYA YA CHEMBA WAHAMASISHWA KUTUMIA FURSA YA KUJIPATIA KIPATO KWA KUTUMIA MIFUGO WALIYONAYO - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WANANCHI WILAYA YA CHEMBA WAHAMASISHWA KUTUMIA FURSA YA KUJIPATIA KIPATO KWA KUTUMIA MIFUGO WALIYONAYO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WANANCHI WILAYA YA CHEMBA WAHAMASISHWA KUTUMIA FURSA YA KUJIPATIA KIPATO KWA KUTUMIA MIFUGO WALIYONAYO
link : WANANCHI WILAYA YA CHEMBA WAHAMASISHWA KUTUMIA FURSA YA KUJIPATIA KIPATO KWA KUTUMIA MIFUGO WALIYONAYO

soma pia


WANANCHI WILAYA YA CHEMBA WAHAMASISHWA KUTUMIA FURSA YA KUJIPATIA KIPATO KWA KUTUMIA MIFUGO WALIYONAYO


Na Shani Amanzi,

Wananchi wa Wilaya ya Chemba wamehamasishwa kutumia fursa ya mifugo waliyonayo katika kuwapatia kipato na siyo kwa ajili ya matumizi ya nyumbani pekee kutokana na mabadiliko ya tabia nchi na wingi wa mahitaji ya kifedha kwa ajili ya shughuli zao za kimaendeleo.

Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi Bw.Simon Langoi aliyazungumza hayo mapema leo 04/12/2018 alipokuwa ofisini kwake Halmashauri ya Wilaya ya Chemba na kueleza changamoto waliyokuwa nayo ni upungufu wa rasilimali watu na upatikanaji hafifu wa chanjo mbalimbali za mifugo(Kichaa cha mbwa,CBPP,CCPP n.k )

Bw. Simon alisema “kumekuwepo na mwitikio mdogo wa Wafugaji katika uchanjaji wa Mifugo yao hasa Mbwa (kichaa cha Mbwa) na Kuku dhidi ya Kideri ,Ukosefu wa Malisho na Maji katika maeneo mbalimbali”.

“Lakini katika maboresho ya mikakati endelevu ya Idara ya Mifugo na Uvuvi kwa Wananchi tumepiga hatua kwa kukinga mifugo dhidi ya magonjwa mbalimbali kama Kichaa cha Mbwa (Rabies) na Kideri kwa Kuku (Newscastle desease) kwa kuwachanja ili kupunguza vifo toka 20% mpaka 10% , kutibu Mifugo na kutoa tiba kwa Mifugo dhidi ya Magonjwa mbalimbali kama FMD, Minyoo na Magonjwa ya Ngozi”.

Kumekuwepo na migogoro baina ya Wakulima na Wafugaji juu ya matumizi bora ya ardhi hasa maeneo ya malisho na kilimo. Halmashauri ya Wilaya ya Chemba kwa kushirikiana na wataalam wa Wizara ya Mifugo,Viongozi wa Serikali za mitaa pamoja na wananchi, imekuwa katika kufanya maamuzi ya pamoja katika kutenga maeneo ya malisho ili kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji.

Wito kwa wafugaji wa Wilaya ya Chemba ni kuhakikisha wanajitokeza kupiga chapa kwa maendeleo ya sekta na pia wanafuga mifugo michache yenye tija na inayoendana na rasilimali zilizopo.

Zoezi la Upigaji Chapa ni endelevu na tayari kwa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba tumefanya zoezi kwa zaidi ya 103% ya lengo, kuelimisha wafugaji wa mbuzi wa maziwa katika vijiji vya Mondo ,Hamai na Songolo ili kuongeza kipato chao na kuboresha lishe zao huku mbinu shirikishi (PPP) ikitumika kati ya Halmashauri na Kanisa la KKKT- Arusha kwenye mradi wa Mbuzi wa Maziwa.

Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi Bw.Simon Langoi akizungumza mapema leo Ofisi kwake,kwa lengo la kuwahamasisha Wananchi wa Wilaya ya Chemba kutumia fursa ya kujipatia kipato kwa kutumia mifugo waliyonayo,mbali ya fursa zilizopo kwa Wananchi hao pia alibanisha baadhi ya changamoto zilizopo ndani ya Idara yake kwa mwaka jana ( 2017)  kuwa ni upungufu wa rasilimali watu pamoja upatikanaji hafifu wa chanjo mbalimbali za mifugo (Kichaa cha mbwa,CBPP,CCPP n.k ) .


Hivyo makala WANANCHI WILAYA YA CHEMBA WAHAMASISHWA KUTUMIA FURSA YA KUJIPATIA KIPATO KWA KUTUMIA MIFUGO WALIYONAYO

yaani makala yote WANANCHI WILAYA YA CHEMBA WAHAMASISHWA KUTUMIA FURSA YA KUJIPATIA KIPATO KWA KUTUMIA MIFUGO WALIYONAYO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WANANCHI WILAYA YA CHEMBA WAHAMASISHWA KUTUMIA FURSA YA KUJIPATIA KIPATO KWA KUTUMIA MIFUGO WALIYONAYO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/wananchi-wilaya-ya-chemba-wahamasishwa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WANANCHI WILAYA YA CHEMBA WAHAMASISHWA KUTUMIA FURSA YA KUJIPATIA KIPATO KWA KUTUMIA MIFUGO WALIYONAYO"

Post a Comment

Loading...