Loading...
title : WANAOOMBA UFADHILI WA MASOMO CHINA, JAPAN WATAHADHARISHWA
link : WANAOOMBA UFADHILI WA MASOMO CHINA, JAPAN WATAHADHARISHWA
WANAOOMBA UFADHILI WA MASOMO CHINA, JAPAN WATAHADHARISHWA
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
MKURUGENZI Mtendaji wa Elimu Solutions (T) Limited Neithan Suedy amesema ni vema Watanzania hasa wanafunzi nchini kuwa makini na matapeli wanaochukua fedha za wanafunzi kwa kigezo cha kuwatafutia vyuo vikuu nje ya nchi.
Amesema wanaungana na Balozi wa Tanzania nchini China kuonya tabia ya baadhi ya mawakala kuchukua fedha za wanafunzi na kisha kushindwa kuwapeleka Kwenye vyuo ambavyo wanaahidi kuwapeleka au kuwapeleka na kusababisha wanafunzi wakifika huko kukosa malazi na makazi.
Akizungumza Dar es Salaam leo, Sissy amesema wenye tabia hiyo wanasababisha matatizo kwa wanafunzi na wanaokwenda huko nchini China wanasababisha mzigo kwa vyuo husika.
"Wanafunzi wanatapeliwa sana na watu hao ambao wanajiita mawakala wa kutafutia ufadhili wanafunzi wa Tanzania kwa vyuo vikuu vya nchini China.
"Ni vema Serikali yetu ikasaidia kudhibiti utapeli huu ambao unafanywa kwa wanafunzi wanaotaka kusoma nchini China, "amesema Suedy.
Akizungumzia kwa upande wao amesema wamekuwa wakitafuta ufadhili kwa wanafunzi wanaohitaji kujiendeleza kielimu nchini China na wanachozingatia wao ni kufuata taratibu ambazo zinatambulika kisheria.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Elimu Solutions Tanzania Ltd, Neithan Swedy akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuanza kwa zoezi la kutuma maombi ya udahili wa masomo kwa wanafunzi wa nje ya nchi (China, Japan na Korea Kusini) pamoja na taratibu mbalimbali zinazopaswa kuzingatiwa na waombaji. Kushoto ni Afisa Tawala wa Taasisi hiyo, Irene Kigwangwa leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Elimu Solutions Ltd, Neithan Swedy akionyesha kwa waandishi wa habari nyaraka ya Namba ya Utambulisho Mlipa Kodi (TIN) inayotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania ( TRA) na kupaswa kuwa nayo kila kampuni ya uwakala wa utafutaji wa nafasi za masomo katika vyuo vya nchi za nje ya Tanzania. Wengine ni Afisa Tawala Irene Kigwanga na Meneja mwendeshaji wa Elimu Solutions, Ibrahim Swedy leo Jijini Dar es Salaam.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WANAOOMBA UFADHILI WA MASOMO CHINA, JAPAN WATAHADHARISHWA
yaani makala yote WANAOOMBA UFADHILI WA MASOMO CHINA, JAPAN WATAHADHARISHWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WANAOOMBA UFADHILI WA MASOMO CHINA, JAPAN WATAHADHARISHWA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/wanaoomba-ufadhili-wa-masomo-china.html
0 Response to "WANAOOMBA UFADHILI WA MASOMO CHINA, JAPAN WATAHADHARISHWA"
Post a Comment