Loading...
title : WATEJA SOKO LA KUKU SHEKILANGO WAPUNGUA
link : WATEJA SOKO LA KUKU SHEKILANGO WAPUNGUA
WATEJA SOKO LA KUKU SHEKILANGO WAPUNGUA
Na Agness Francis, Globu ya Jamii
WAFANYABIASHARA wa kuku katika soko la Kuku lililopo Shekilango jijini Dar es Salaam wamesema kwa sasa soko limekuwa gumu kidogo kutokana na kupungua kwa wateja tofauti na siku za nyuma.
Wakizungumza na Michuzi Blog, leo sokoni hapo ,wafanyabishara hao wamesema hali hiyo imewafanya wawe katika wakati mgumu kurudisha faida.
Mmoja wa wafanyabishara wa kuku sokoni hapo Mussa Shaaban amesema changamoto ya wateja wa kuku kupungua imekuwa kubwa na hivyo kijikuta wakiwa na hali ngumu kiuchumi kwani kuku hao kabla ya kununuliwa wanahitaji kuhudumiwa na hiyo nayo inahitaji gharama yake.
Pia amesema changamoto nyingine kwenye biashara hiyo ni baadhi ya kuku kufia njiani kutokana na umbali mrefu wanaotumia wakati wa kuwasafirisha hadi kufika sokoni hapo kwani wanawanunua mikoani.
Kuhusu bei, amesema wao wananunua kuku wa kienyeji kwa Sh 13,500 hadi Sh 14, 000 na kisha wao huuza kuku mmoja kwa Sh 18,000 hadi Sh.20,000. Pia amesema kwa kuku wa kisasa wamekuwa wakiwauza kwa Sh 6,300.
Pia imeelezwa na wafanyabishara hao kuku wa mayai wao wananunua kuku mmoja kwa Sh 8,000 hadi Sh 8,500 na kisha wanawauza kwa reja reja kwa Sh10,000 na kwa jumla wanauza Sh 9000 hadi Sh.9500.
Hivyo makala WATEJA SOKO LA KUKU SHEKILANGO WAPUNGUA
yaani makala yote WATEJA SOKO LA KUKU SHEKILANGO WAPUNGUA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WATEJA SOKO LA KUKU SHEKILANGO WAPUNGUA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/wateja-soko-la-kuku-shekilango-wapungua.html
0 Response to "WATEJA SOKO LA KUKU SHEKILANGO WAPUNGUA"
Post a Comment