Loading...

WATOTO YATIMA 150 WAPATIWA MSADA WA VIFAA VYA SHULE

Loading...
WATOTO YATIMA 150 WAPATIWA MSADA WA VIFAA VYA SHULE - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WATOTO YATIMA 150 WAPATIWA MSADA WA VIFAA VYA SHULE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WATOTO YATIMA 150 WAPATIWA MSADA WA VIFAA VYA SHULE
link : WATOTO YATIMA 150 WAPATIWA MSADA WA VIFAA VYA SHULE

soma pia


WATOTO YATIMA 150 WAPATIWA MSADA WA VIFAA VYA SHULE

Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (mwenye nguo ya njano), Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji Mdogo Gairo, Mhe. Andrea Sendeha (wa tatu toka kulia) pamoja na kamati ya ulinzi na usalama wakiwa katika picha ya pamoja na watoto yatima wa kituo cha Bethel wa Gairo.

 Katika kujali makundi yenye changamoto za maisha hasa watoto wadogo, Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Shaidi Mchembe amegawa sare za shule na madaftari kwa watoto yatima 150 kituo cha Bethel Wilayani Gairo kinachosimamiwa na Mchungaji Chacha. Hafla hiyo ya ugawaji wa vifaa ulifanyika mapema wiki hii, ambapo Mhe. 

Mchembe amesema kuwa huo ni utamaduni aliojiwekea kila mwanzo wa mwaka wa kuwakumbuka watoto yatima na wale waishi katika mazingira magumu. "Nawakumbusha wananchi kujenga utamaduni wa kusaidiana watu wasiojiweza ili muweze kupata baraka kutoka kwa mwenyezi Mungu, unajua unapokuwa nacho ukatoa kidogo unabarikiwa zaidi," alisema Mhe. Mchembe. 

Mhe. Mchembe aliwakumbusha watoto hao kuzingatia masomo kwani Serikali ya awamu ya tano ya Dr. John Magufuli inatoa elimu bure hivyo hakuna mtoto wa masikini atakayeshindwa kusoma. Katika kukua kwao wamtangulize Mungu naye ataendelea kuwabariki na kuwatoa katika hali ya kuhisi unyonge wa kukosa wazazi. Mwisho aliwaasa waalimu kuwa na moyo wa upendo kwa watoto yatima. Pia kuweka karibu hasa watoto wa kike kuwaepusha na mimba za utotoni.
 Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe akiwaasa watoto yatima wa kituo cha Bethel Wilayani Gairo. Kulia kwake ni baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama walioambatana naye.  Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji Mdogo Gairo, Mhe. Andrea Sendeha akitoa salamu kwa watoto yatima. 

Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe akigawa zawadi kwa watoto yatima wa kituo cha Bethel kilichopo wilayani humo. 
Watoto wa kituo cha Bethel Wilayani Gairo wakiwa wamejipanga mstari kupokea zawadi. 


Hivyo makala WATOTO YATIMA 150 WAPATIWA MSADA WA VIFAA VYA SHULE

yaani makala yote WATOTO YATIMA 150 WAPATIWA MSADA WA VIFAA VYA SHULE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WATOTO YATIMA 150 WAPATIWA MSADA WA VIFAA VYA SHULE mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/watoto-yatima-150-wapatiwa-msada-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WATOTO YATIMA 150 WAPATIWA MSADA WA VIFAA VYA SHULE"

Post a Comment

Loading...