Loading...

WIZARA YA ELIMU YATOA VITABU 16985 KWA SHULE ZA SEKONDARI SIMIYU

Loading...
WIZARA YA ELIMU YATOA VITABU 16985 KWA SHULE ZA SEKONDARI SIMIYU - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WIZARA YA ELIMU YATOA VITABU 16985 KWA SHULE ZA SEKONDARI SIMIYU, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WIZARA YA ELIMU YATOA VITABU 16985 KWA SHULE ZA SEKONDARI SIMIYU
link : WIZARA YA ELIMU YATOA VITABU 16985 KWA SHULE ZA SEKONDARI SIMIYU

soma pia


WIZARA YA ELIMU YATOA VITABU 16985 KWA SHULE ZA SEKONDARI SIMIYU

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(kushoto) akikabidhi vitabu vya matayarisho ya awali ya kuwaandaa wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa elimu ya sekondari (baseline course), kwa Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Mji Bariadi, Mwl. Esthom Makyara vilivyotolewa na wadau wa Elimu, wakati wa zoezi la ugawaji wa vitabu hivyo lililofanyika kimkoa Mjini Bariadi.

Na Stella Kalinga, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu

Wizara ya Elimu pamoja na wadau wengine wa Elimu wametoa vitabu 16,985 kwa shule za Sekondari za Mkoa wa Simiyu kwa ajili ya  matayarisho ya awali ya kuwaandaa wanafunzi wa kidato cha kwanza na elimu ya sekondari (baseline course).

Akikabidhi vitabu hivyo kwa Maafisa Elimu wa Halmashauri zote sita za Mkoa wa Simiyu, Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka amesema vitabu hivyo ni msaada mkubwa kwa Mkoa huo, vikitumiwa vizuri na walimu wenye nia ya kufanya mapinduzi ya elimu na kuwasaidia wanafunzi kujua maana halisi ya vitabu hivyo, vitasaidia  Mkoa wa Simiyu kufikia malengo ya kiushindani katika Elimu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na Maafisa Elimu Sekondari na baaadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Bariadi(hawapo pichani), kabla ya kukabidhi vitabu vya matayarisho ya awali ya kuwaandaa wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa elimu ya sekondari (baseline course), kwa maafisa elimu wilaya vilivyotolewa na wadau mbaimbali wa Elimu.

Ameongeza kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata vitabu pamoja na mahitaji mengine ikiwa ni pamoja na madawati, walimu, vyumba vya madarasa vinavyotolesheleza hivyo akasisitiza vitabu hivyo vikatumike kwa kusoma ili viwasaidie. “Vitabu hivi mtakapogawiwa mkavitumie kwa ajili ya kusoma visiwe mapambo na kama mwanafunzi hujui uliza, jibidiishe kujua kitabu hicho kinahusu nini na kama hujaelewa muulize mwalimu ili kesho kwenye mtihani ufaulu kama wenzako wananvyofaulu” alisema Mtaka.

Aidha, Mtaka amewataka Maafisa Elimu mkoani humo kuzungumza na walimu kabla ya kugawa vitabu hivyo ili vitakapogawiwa katika shule vigawiwe katika utaratibu mzuri utakowawezesha walimu kuwasadia wanafunzi kuvitumia kwa manufaa. Akitoa taarifa juu mapokezi ya vikao hivyo Katibu Tawala Mkoa amesema Mkoa huo umepokea jumla ya vitabu 16,000 kwa ajili ya wanafunzi na vitabu 985 kwa ajili walimu(kiongozi cha mwalimu).
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(kushoto) akikabidhi vitabu vya matayarisho ya awali ya kuwaandaa wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa elimu ya sekondari (baseline course), kwa Afisa Elimu (Sekondari) wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Mwl. Jumanne Yasini vilivyotolewa na wadau wa Elimu, wakati wa zoezi la ugawaji wa vitabu hivyo lililofanyika kimkoa Mjini Bariadi.

Akizungumza kwa niaba ya Maafisa Elimu Sekondari mkoani humo,  Afisa Elimu Sekondari wa Halmahauri ya Mji Bariadi Mwl. Esthom Makyara amesema vitabu hivyo ni msingi mzuri kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza na Maafisa Elimu hao wanapaswa  kuwaelekezaWakuu wa shule kutofungia vitabu hivyo  stoo badala yake wanafunzi wapewe ili wavisome.

Naye Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Simiyu, Ndg.Charles Maganga amesema Maafisa Elimu Sekondari wahakikishe vitabu hivyo vinagawiwa kwa wakuu wa shule kabla ya shule kufunguliwa Januari 08, 2018, ili wanafunzi wa kidato cha kwanza wanapoanza masomo wavikute shuleni. Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Bariadi walioshuhudia zoezi la ugawaji wa vitabu hivyo kimkoa wamesema, vitabu hivyo vitawasaidia wenzao wa kidato cha kwanza kujenga msingi  mzuri wa maarifa ya jumla na lugha ya Kiingereza.

Vitabu hivi vimetolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Msaada wa Watu wa Marekani(UKAID) kupitia Mpango wa Taifa wa Kuinua Ubora wa Elimu hapa nchini EQUIP-T.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(kushoto) akikabidhi vitabu vya matayarisho ya awali ya kuwaandaa wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa elimu ya sekondari (baseline course), kwa Afisa Elimu (Sekondari) wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Mwl. Joseph Mashauri vilivyotolewa na wadau wa Elimu, wakati wa zoezi la ugawaji wa vitabu hivyo lililofanyika kimkoa Mjini Bariadi.


Hivyo makala WIZARA YA ELIMU YATOA VITABU 16985 KWA SHULE ZA SEKONDARI SIMIYU

yaani makala yote WIZARA YA ELIMU YATOA VITABU 16985 KWA SHULE ZA SEKONDARI SIMIYU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WIZARA YA ELIMU YATOA VITABU 16985 KWA SHULE ZA SEKONDARI SIMIYU mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/wizara-ya-elimu-yatoa-vitabu-16985-kwa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WIZARA YA ELIMU YATOA VITABU 16985 KWA SHULE ZA SEKONDARI SIMIYU"

Post a Comment

Loading...