Loading...
title : DC MJEMA AKAGUA MIRADI YA DMDP WILANI ILALA,APIGA MARUFUKU WANAO PANGA VITU KATIKA MAENEO YA UJENZI
link : DC MJEMA AKAGUA MIRADI YA DMDP WILANI ILALA,APIGA MARUFUKU WANAO PANGA VITU KATIKA MAENEO YA UJENZI
DC MJEMA AKAGUA MIRADI YA DMDP WILANI ILALA,APIGA MARUFUKU WANAO PANGA VITU KATIKA MAENEO YA UJENZI
MwambawahabariMkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema leo ametembelea maeneo mbalimbali ndani ya Wilaya hiyo na kukagua maendeleo ya mradi wa DMDP ambao ni mradi wa maendeleo ndani ya jiji la Dar es salaam unaohusisha jumla ya Wilaya nne ndani ya jiji ambazo ni Temeke, Ilala na Kinondoni, unategemewa kukamilika februari 27 mwaka huu.
Akiongea na waandishi wa habari Dc Mjema amesema katika mradi huo kutajengwa barabara takribani nne pamoja na jengo moja ambalo litatumika kama maabara kwa ajili ya kupima kokoto na udongo utakaokuwa unatumika katika ujenzi wa barabara hizo na kutumika kwa ajili ya mikutano ya wahandisi watakaohusika katika ujenzi huo.
Amesema barabara zitakazojengwa ni barabara ya Ndanda yenye kilometa 0.35, barabara ya Ulimpio kilometa 0.86, barabara ya kiungani kilometa 0.70 na barabara ya paruku yenye kilometa 0.40 ambazo kwa ujumla zimegharimu bilioni 11 huku jengo likigharimu bilioni 1.
Ameongeza kuwa pamoja na mradi huo kuendelea vizuri bado kuna changamoto kwa baadhi ya maeneo ambapo wafanyabiashara wanafanya biashara eneo la barabara huku ujenzi ukiwa unaendelea hivyo amewaomba wananchi kupenda barabara zao ili kwa pamoja waweze kufikia lengo kwani itawasaidia hata wao wenyewe kufanya biashara katika mazingira mazuri pasipo na vumbi.
Kwa upande wake mhandisi kutoka manispaa ya ilala Mboya amesema kuwa ujenzi wa jengo litakalotumika kwa ajili ya vipimo vya kokoto na udongo itasaidia na kuleta ufanisi katika ujenzi wa barabara na kuongeza kuwa itasaidia pia katika majaribio kwani itapelekea kupata matokeo kwa muda mfupi na kazi kutendeka kwa muda muafaka.
Pia mwananchi mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Abubakhari Said amesema kuwa wameupokea mradi huo kwa furaha kubwa kwani umeweza kutatua changamoto ya maji kujaa wakati wa mvua na kuahidi kwamba watashirikiana na serikali kukemea wafanyabiashara wanaoweka biashara zao pembezoni mwa barabara.Hivyo makala DC MJEMA AKAGUA MIRADI YA DMDP WILANI ILALA,APIGA MARUFUKU WANAO PANGA VITU KATIKA MAENEO YA UJENZI
yaani makala yote DC MJEMA AKAGUA MIRADI YA DMDP WILANI ILALA,APIGA MARUFUKU WANAO PANGA VITU KATIKA MAENEO YA UJENZI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC MJEMA AKAGUA MIRADI YA DMDP WILANI ILALA,APIGA MARUFUKU WANAO PANGA VITU KATIKA MAENEO YA UJENZI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/dc-mjema-akagua-miradi-ya-dmdp-wilani.html
0 Response to "DC MJEMA AKAGUA MIRADI YA DMDP WILANI ILALA,APIGA MARUFUKU WANAO PANGA VITU KATIKA MAENEO YA UJENZI"
Post a Comment