Loading...
title : FARM AFRICA YAHAMASISHA WAKULIMA WADOGO WA NAFAKA KUTUMIA MITANDAO KUPATA MASOKO YA MAZAO
link : FARM AFRICA YAHAMASISHA WAKULIMA WADOGO WA NAFAKA KUTUMIA MITANDAO KUPATA MASOKO YA MAZAO
FARM AFRICA YAHAMASISHA WAKULIMA WADOGO WA NAFAKA KUTUMIA MITANDAO KUPATA MASOKO YA MAZAO
Na Mwandishi Wetu, Arusha
Shirika la Kimataifa la Farm Africa limewataka wakulima wadogo wa mazao ya nafaka hapa nchini kutumia mifumo ya mitandao kupitia simu za mkononi kutangaza bei ya mazao ya nafaka na kupata taarifa za kilimo bora ili kuwasaidia kupata kipato chenye tija na kuondokana na hali duni katika familia zao.
Meneja Program ya FoodTrade wa Shirika hilo la Kimataifa la Farm Africa,Bi. Beatrice Muliahela alisema hayo jijini Arusha katika warsha ya siku moja kuwa wakulima wadogo wanahitajika kutumia mifumo ya mitandao kupitia simu katika kutangaza bei ya mazao yao na kupata taarifa za kilimo bora ili kuwasaidia kupata kipato chenye tija na kuondokana na hali duni katika familia zao.
Mradi huu ni wa miaka miwili na unafadhiliwa na Department for International Development (DFID) kupitia DAI kwa kuhusisha wadau wengine kama Taasisi ya Maendeleo Vijijini na Mijini (RUDI) na VECO kwa sasa Rikolto ambao umesaidia wakulima wadogo 70,000 nchini Tanzania na Uganda.
“Farm Africa inahitaji kuona wakulima wadogo nchini Tanzania wanatumia mifumo ya mitandao kupitia simu katika kutangaza bei ya mazao yao na kuuza kwa bei nzuri zaidi,” na hii tunahamasisha katika nchi zote kumi za Afrika Mashariki kutumia mifumo hii, aliongeza kusema,Bi. Muliahela.
Mkurugenzi wa Msaidizi Kitengo cha Kuzuia Upotevu wa Mazao baada ya Mavuno Wizara ya Kilimo, Bi. Josephine Omolo kushoto akifuatilia mada katika warsha iliyokuwa ikizungumzia jinsi wakulima wanavyoweza kutumia mifumo ya mitandao kupitia simu za mkononi kutangaza bei ya mazao yao na kupata taarifa za kilimo bora na kipato chenye tija kuwawezesha kuondokana na hali duni katika familia zao, katikati ni Meneja Program ya FoodTrade wa Shirika la Kimataifa la Farm Africa,Bi. Beatrice Muliahela na kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Maendeleo Vijijini na Mijini (RUDI), Lameck Kikoka.
Wadau wa Shirika la Kimataifa la Farm Africa wanaojihusisha na shughuli za kilimo wakifuatilia mada katika warsha iliyokuwa ikizungumzia jinsi wakulima wanavyoweza kutumia mifumo ya mitandao kupitia simu za mkononi kutangaza bei ya mazao yao na kupata taarifa za kilimo bora na kupata kipato chenye tija kuwezesha kuondokana na hali duni katika familia zao.
Meneja Program ya FoodTrade wa Shirika la Kimataifa la Farm Africa,Bi. Beatrice Muliahela akifafanua jambo katika warsha iliyokuwa ikizungumzia jinsi wakulima wanavyoweza kutumia mifumo ya mitandao kupitia simu za mkononi kutangaza bei ya mazao yao na kupata taarifa za kilimo bora kupata kipato chenye tija na kuondokana na hali duni katika familia zao, katikati ni Mkurugenzi wa Msaidizi Kitengo cha Kuzuia Upotevu wa Mazao baada ya Mavuno Wizara ya Kilimo, Bi. Josephine Omolo na kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Maendeleo Vijijini na Mijini (RUDI), Lameck Kikoka.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala FARM AFRICA YAHAMASISHA WAKULIMA WADOGO WA NAFAKA KUTUMIA MITANDAO KUPATA MASOKO YA MAZAO
yaani makala yote FARM AFRICA YAHAMASISHA WAKULIMA WADOGO WA NAFAKA KUTUMIA MITANDAO KUPATA MASOKO YA MAZAO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala FARM AFRICA YAHAMASISHA WAKULIMA WADOGO WA NAFAKA KUTUMIA MITANDAO KUPATA MASOKO YA MAZAO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/farm-africa-yahamasisha-wakulima-wadogo.html
0 Response to "FARM AFRICA YAHAMASISHA WAKULIMA WADOGO WA NAFAKA KUTUMIA MITANDAO KUPATA MASOKO YA MAZAO"
Post a Comment