Loading...

KAMISHNA MKUU WA TRA AMSIMAMISHA KAZI MENEJA WA TRA MKOA WA MARA

Loading...
KAMISHNA MKUU WA TRA AMSIMAMISHA KAZI MENEJA WA TRA MKOA WA MARA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa KAMISHNA MKUU WA TRA AMSIMAMISHA KAZI MENEJA WA TRA MKOA WA MARA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : KAMISHNA MKUU WA TRA AMSIMAMISHA KAZI MENEJA WA TRA MKOA WA MARA
link : KAMISHNA MKUU WA TRA AMSIMAMISHA KAZI MENEJA WA TRA MKOA WA MARA

soma pia


KAMISHNA MKUU WA TRA AMSIMAMISHA KAZI MENEJA WA TRA MKOA WA MARA


Na: Veronica Kazimoto-Bunda, 

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere amemsimamisha kazi Meneja wa TRA Mkoa wa Mara Ndg. Nicodemus Mwakilembe kutokana na uzembe wa kutosimamia vizuri matumizi ya Mashine za Kielektroniki za Kutolea Risiti (EFDs) kwa wafanyabiashara wa mkoani kwake. 

Uamuzi huo umetokana na ziara ya kushtukiza ya kukagua matumizi ya EFD aliyoifanya Kamshina Mkuu wa TRA kwenye baadhi ya maduka ya biashara Wilayani Bunda Mkoa wa Mara. Akizungumza mara baada ya ziara yake, Kamishna Mkuu Kichere alisema Meneja huyo ameonyesha uzembe wa hali ya juu kwani kuna wafanyabishara wengi mkoani kwake ambao walishalipa fedha kwa ajili ya kupata mashine za EFD lakini mpaka sasa hawajapatiwa mashine hizo. 

"Katika ziara yangu nimegundua kwamba, wapo wafanyabiashara ambao walikwisha kulipia mashine tangu mwaka 2013, 2014 na 2015 lakini mpaka sasa bado hawajapatiwa mashine za EFD na wamekuwa wakitumia mwanya huo kama kinga ya kutochukuliwa adhabu na TRA wakati Meneja wa Mkoa yupo na hachukui hatua zozote. Huu ni uzembe uliopitiliza na kamwe siwezi kuuvumilia," alisema Kichere. 

Kutokana na uzembe huo, Kamishna Mkuu Kichere amewaagiza Mameneja wote wa TRA nchi nzima pamoja na majukumu mengine, kuhakikisha wanasimamia kikamilifu matumizi ya mashine za EFD katika mikoa yao na amesema hatasita kumuwajibisha Meneja yeyote atakayeshindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo. 
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (kulia) akimsisitizia jambo Mfanyabiashara wa duka la nguo Wilayani Bunda Mkoani Mara kuhusu suala la umuhimu wa kutumia mashine ya Kielektroniki ya Kutolea Risiti (EFD) mara alipofanya ukaguzi wa mashine hizo katika baadhi ya maduka Wilayani hapo 3 Februari, 2018.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (kulia) akikagua taarifa ya mauzo ya siku ya Mashine ya Kielektroniki ya Kutolea Risiti (EFD) toka kwa Wafanyabiashara wa duka la vifaa vya nyumbani Wilayani Bunda Mkoani Mara mara alipofanya ukaguzi wa mashine hizo katika baadhi ya maduka Wilayani hapo 3 Februari, 2018.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (aliyekaa mbele) akiongea na kutoa maagizo kwa Meneja wa TRA Wilaya ya Bunda Mkoani Mara pamoja na wafanyakazi wengine wa Mamlaka hiyo kuhusu ukusanyaji wa mapato ya Serikali mara alipotembelea ofisi ya TRA Wilayani hapo ili kujionea namna ukusanyaji mapato unavyofanyika mapema 3 Februari, 2018.



Hivyo makala KAMISHNA MKUU WA TRA AMSIMAMISHA KAZI MENEJA WA TRA MKOA WA MARA

yaani makala yote KAMISHNA MKUU WA TRA AMSIMAMISHA KAZI MENEJA WA TRA MKOA WA MARA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala KAMISHNA MKUU WA TRA AMSIMAMISHA KAZI MENEJA WA TRA MKOA WA MARA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/kamishna-mkuu-wa-tra-amsimamisha-kazi_4.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "KAMISHNA MKUU WA TRA AMSIMAMISHA KAZI MENEJA WA TRA MKOA WA MARA"

Post a Comment

Loading...