Loading...
title : KANALI NDAGALA AKABIDHI MABATI 280 KWA WALIMU 14 WALIOSTAAFU KAKONKO
link : KANALI NDAGALA AKABIDHI MABATI 280 KWA WALIMU 14 WALIOSTAAFU KAKONKO
KANALI NDAGALA AKABIDHI MABATI 280 KWA WALIMU 14 WALIOSTAAFU KAKONKO
Na Rhoda Ezekiel Kigoma,
MKUU wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala amekabidhi mabati 280 kwa wastaafu 14.
Amekabidhi mabati hayo kwa niaba ya kamati tendaji ya Chama cha Waalimu Tanzania(CWT)Wilaya ya Kakonko ambayo ni zawadi kwa kufanya kazi iliyotukuka kwa kipindi chote cha utumishi wao.
Akikabidhi mabati hayo juzi kwa wastaafu katika ofisi za CWT wilayani Kakonko Kanali Ndagala aliwapongeza wastaafu hao na kuwasisitiza kutumia zawadi waliyopewa kukamilisha nyumba zao au kuanzisha biashara itakayowasaidia kuendeleza maisha yao.
Amesema kila mhsataafu amepewa mabati 20 kama zawadi za pongezi kutokana uadilifu.Pia pamoja na kujituma wakati wakiitumikia Serikali katika sekta ya elimu ambapo chama hicho kimetambua utendaji wao uliotukuka.
“Niwapongeze kwa kumaliza salama muda wenu, mnapoenda kuanza maisha mapya na mazuri, huu ni mwanzo mzuri kama hujamalizia kibanda kamalizie."Kama tayari ni vizuri kujenga kibanda cha biashara au kufuga ilikuweza kujikimu kwa kipindi hiki maana kuna maisha baada ya kustaafu,”, amesema Kanali Ndagala.
MKUU wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala akikabidhi mabati 280 kwa mmoja wa wastaafu kati ya 14.Ndagaka amekabidhi mabati hayo kwa niaba ya kamati tendaji ya Chama cha Waalimu Tanzania (CWT) Wilaya ya Kakonko ambayo ni zawadi kwa kufanya kazi iliyotukuka kwa kipindi chote cha utumishi wao.
Baadhi ya Wastaafu hao hao wakimsikiliza MKUU wa Wilaya ya Kakonko Kanali (hayupo pichani),Hosea Ndagala mara baada ya kuwakabidhi mabati 280.
Hivyo makala KANALI NDAGALA AKABIDHI MABATI 280 KWA WALIMU 14 WALIOSTAAFU KAKONKO
yaani makala yote KANALI NDAGALA AKABIDHI MABATI 280 KWA WALIMU 14 WALIOSTAAFU KAKONKO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KANALI NDAGALA AKABIDHI MABATI 280 KWA WALIMU 14 WALIOSTAAFU KAKONKO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/kanali-ndagala-akabidhi-mabati-280-kwa.html
0 Response to "KANALI NDAGALA AKABIDHI MABATI 280 KWA WALIMU 14 WALIOSTAAFU KAKONKO"
Post a Comment