Loading...

LUNDENGA ATANGAZA KUBWAGA MANYANGA KUANDAA MASHINDANO MISS TANZANIA

Loading...
LUNDENGA ATANGAZA KUBWAGA MANYANGA KUANDAA MASHINDANO MISS TANZANIA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa LUNDENGA ATANGAZA KUBWAGA MANYANGA KUANDAA MASHINDANO MISS TANZANIA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : LUNDENGA ATANGAZA KUBWAGA MANYANGA KUANDAA MASHINDANO MISS TANZANIA
link : LUNDENGA ATANGAZA KUBWAGA MANYANGA KUANDAA MASHINDANO MISS TANZANIA

soma pia


LUNDENGA ATANGAZA KUBWAGA MANYANGA KUANDAA MASHINDANO MISS TANZANIA


Na Leandra Gabriel , Globu ya Jamii

MKURUGENZI wa Kampuni inayoandaa mashindano ya Miss Tanzania ya Lino International Agency LTD Hashim Lundenga ametangaza rasmi kuacha shughuli za kuendesha mashindano hayo kuanzia Februari 13 mwaka huu.

Hivyo kuanzia sasa mashindano ya Miss Tanzania nchini yataendeshwa na The Look Company Limited, chini ya Mkurugenzi Basila Mwanukuzi aliyewahi kuwa Miss Tanzania mwaka 1998.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Hashim Lundenga amesema uamuzi huo umetokana na malengo yao ya kutaka mashindino hayo kusimamiwa na damu changa kwa lengo la kuleta chachu katika tasnia ya urembo nchini.

“Tumefikia uamuzi huu baada ya kuona kampuni yetu tayari imejijengea sifa na heshima nchini.Hata hivyo tunaamini The Look Company Limited chini ya Mkurugenzi Mwanukuzi watasimamia taratibu, kanuni, sheria na miiko ya uongozi na hatimaye kumpeleka mrembo katika mashindano ya dunia kama ilivyo kawaida,”amesema. Amewataka waandaaji wapya wa mashindano ya urembo wasisite kuomba ushauri au mawazo ya kujenga kutoka kwao pale watakapohitaji.

Lundenga ambaye ni maarufu kama Uncle Hashim amewashukuru Baraza za sanaa la Taifa (BASATA), na Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo kwa ushirikiano mkubwa kwa muda wote tangu kuanza kwa mashindano hayo mwaka 1994.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Look Limited, Mwanukuzi amesema wamejiwekea mikakati kuendeleza fani ya ulimbwende pale ambapo kampuni ya Lino imeishia. Amesema kuwa pale penye changamoto katika kuandaa masuala ya warembo watakuwa karibu na Kampuni ya Lino pamoja na BASATA ili kufanikisha na kuleta tija katika Taifa.
 MKURUGENZI wa Kampuni inayoandaa mashindano ya Miss Tanzania ya Lino International Agency LTD Hashim Lundenga akitangaza uamuzi wake rasmi kuacha shughuli za kuendesha mashindano hayo kuanzia Februari 13 mwaka huu,pichani kati ni Mkurugenzi wa The Look Company Limited Basila Mwanukuzi pamoja na Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA),Godrey Mngereza akishuhudia tukio hilo.
 Mkurugenzi wa The Look Company Limited Basila Mwanukuzi akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari mapema leo jijini Dar,wakati akikabidhiwa jukumu la kuendesha shughuli za shindalo la Miss Tanzania


Hivyo makala LUNDENGA ATANGAZA KUBWAGA MANYANGA KUANDAA MASHINDANO MISS TANZANIA

yaani makala yote LUNDENGA ATANGAZA KUBWAGA MANYANGA KUANDAA MASHINDANO MISS TANZANIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala LUNDENGA ATANGAZA KUBWAGA MANYANGA KUANDAA MASHINDANO MISS TANZANIA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/lundenga-atangaza-kubwaga-manyanga.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "LUNDENGA ATANGAZA KUBWAGA MANYANGA KUANDAA MASHINDANO MISS TANZANIA"

Post a Comment

Loading...