Loading...

MANAIBU WAZIRI MAVUNDE NA BITEKO WAFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA MGODI WA ALMASI MJINI SHINYANGA.

Loading...
MANAIBU WAZIRI MAVUNDE NA BITEKO WAFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA MGODI WA ALMASI MJINI SHINYANGA. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MANAIBU WAZIRI MAVUNDE NA BITEKO WAFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA MGODI WA ALMASI MJINI SHINYANGA., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MANAIBU WAZIRI MAVUNDE NA BITEKO WAFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA MGODI WA ALMASI MJINI SHINYANGA.
link : MANAIBU WAZIRI MAVUNDE NA BITEKO WAFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA MGODI WA ALMASI MJINI SHINYANGA.

soma pia


MANAIBU WAZIRI MAVUNDE NA BITEKO WAFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA MGODI WA ALMASI MJINI SHINYANGA.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana, Mhe. Antony Mavunde, na Naibu Waziri Madini Mhe. Dotto Biteko, leo Jumanne Februari 27,2018 wamefanya ziara ya kushtukiza kwenye mgodi wa almasi wa El – Hilal Minerals Limited uliopo katika kijiji cha Maganzo kata ya Maganzo wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga. 
 
Manaibu Waziri hao walikuwa wameambatana na maafisa kutoka WCF na Ofisi ya Kazi ,lengo la ziara hiyo ikiwa ni kubaini kama wamiliki wa mgodi huo wanatekeleza sheria za uendeshaji. 
 
Wakati Mheshimiwa Mavunde alikuwa akifuatilia kama mgodi huo umejisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi (Workers Compensation Fund -WCF), Mhe. Biteko alikuwa akifuatilia kwa nini mgodi huo haujawasilisha wizarani mpango wa ukarabati wa mazingira (rehabilitation plan) na mpango wa uwajibikaji wa shirika kwa jamii (Corporate Social Responsibility-CSR). 
 
Akiwa katika mgodi huo Mhe. Mavunde alibaini kuwa Mgodi huo bado ulikuwa haujajisajili na Mfuko wa WCF na badala yake uongozi ulipeleka michango siku moja kabla ya ziara ya Naibu waziri huyo kufika katika mgodi huo. 
 
“Serikali inataka waajiri wazingatie sheria, na ninyi mmevunja sheria kwa kutojisajili, ingawa mmelipa michango yenu jana, ninachoweza kusema, agizo la serikali la kuwafikisha mahakamani waajiri ambao hawajajisajili nchi nzima liko pale pale, ni juu yenu kutekeleza hilo kabla hamjapelekwa mahakamani”, alisema Mhe. Mavunde. 
 
Mh. Mavunde pia alibaini kuwa mgodi huo hautoi mikataba ya kudumu kwa wafanyakazi,wafanyakazi kufanyishwa kazi zaidi ya muda wa kazi bila malipo,wafanyakazi kutopewa vifaa kinga na mishahara kutolipwa kwa wakati na kuwaagiza kurekebisha mapungufu yaliyopo kwenye mgodi huo ndani ya siku 30. 
 
“Nawapa siku 14 za kujisajili WCF na kurekebisha mapungufu yaliyopo hapa ndani ya siku 30,ni lazima tutii na kuziheshimu sheria zetu wanaokiuka sheria tunawafikisha mahamani”,alisema Mhe. Mavunde. 
 
Ziara ya Naibu Waziri Mavunde ni muendelezo wa ziara yake iliyoanza Februari 26, 2018 jijini Mwanza ambapo aliagiza kufikishwa mahakamani waajiri watatu jijini Mwanza ambao hawajajisajili katika mfuko wa WCF. 
 
Mhe. Mavunde ameagiza waajiri hao kufanya mawasiliano na watendaji wa Mfuko haraka iwezekanavyo ili kuweza kubaini kiwango cha riba kila mwajiri anachopaswa kulipa kutokana na kuchelewesha michango katika Mfuko. 
 
“Ni kosa la jinai kwa mwajiri kutotekelza takwa hilo la kisheria na kifungu cha 71(4) cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi kimeweka wazi kuwa mwajiri wa aina hii, anaweza kutozwa faini isiyozidi shilingi milioni 50,000, kifungo kisichozidi miaka 5 jela au adhabu zote kwa pamoja,Nitoe wito kwa waajiri hao, hakuna sababu ya kushurutishwa kutekeleza sheria­”,alisema.


Hivyo makala MANAIBU WAZIRI MAVUNDE NA BITEKO WAFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA MGODI WA ALMASI MJINI SHINYANGA.

yaani makala yote MANAIBU WAZIRI MAVUNDE NA BITEKO WAFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA MGODI WA ALMASI MJINI SHINYANGA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MANAIBU WAZIRI MAVUNDE NA BITEKO WAFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA MGODI WA ALMASI MJINI SHINYANGA. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/manaibu-waziri-mavunde-na-biteko.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MANAIBU WAZIRI MAVUNDE NA BITEKO WAFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA MGODI WA ALMASI MJINI SHINYANGA."

Post a Comment

Loading...