Loading...

MAVUNDE ASISITIZA ELIMU ZAIDI JUU YA TATIZO LA USUGU WA VIMELEA VYA DAWA

Loading...
MAVUNDE ASISITIZA ELIMU ZAIDI JUU YA TATIZO LA USUGU WA VIMELEA VYA DAWA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAVUNDE ASISITIZA ELIMU ZAIDI JUU YA TATIZO LA USUGU WA VIMELEA VYA DAWA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAVUNDE ASISITIZA ELIMU ZAIDI JUU YA TATIZO LA USUGU WA VIMELEA VYA DAWA
link : MAVUNDE ASISITIZA ELIMU ZAIDI JUU YA TATIZO LA USUGU WA VIMELEA VYA DAWA

soma pia


MAVUNDE ASISITIZA ELIMU ZAIDI JUU YA TATIZO LA USUGU WA VIMELEA VYA DAWA


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde amesisitiza kuwepo kwa kampeni kubwa ya nchi nzima juu Elimu ya tatizo la Usugu wa vimelea vya dawa.

Mavunde ameyasema hayo leo wakati akihitimisha kampeni ya Elimu ya Tatizo la Usugu wa vimelea vya dawa katika Shule ya Sekondari ya Wasichana-Msalato,Dodoma ambapo ametumia fursa hiyo kuwataka wadau na taasisi mbalimbali za umma na binafsi kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Chama cha Wanafunzi Wafamasia Tanzania(TASPA) ambao wamejitolea kutembea nchi nzima kutoa elimu.

“Najua moja kati ya sababu nyingi zinazosababisha usugu wa vimelea vya madawa ni ubora hafifu wa dawa na utoaji wa dawa pasipo cheti cha daktari”amesema Mavunde.Kufuatia hali hiyo, Mavunde ametumia nafasi hiyo kwa kuzitaka Taasisi za TFDA na Baraza la Wafamasia Tanzania kuchukua hatua kali na stahiki kwa wale wote wanaovunja sheria na miongozo iliyowekwa katika kusimamia masuala yote ya dawa na tiba.

Akimkaribisha Mgeni Rasmi, Rais wa TASPA Erick Venant ameeleza kwamba kampeni hiyo ya kujitolea wamefanya nchi nzima kwa mikoa 23 na Shule za Sekondari 123 na wamewafikia takriban watanzania 6 milioni.

Venant amesisitiza kwamba tatizo hili ni hatari kuliko hata ugonjwa wa UKIMWI kwa kuwa takribani watu 700,000 wanafariki kila mwaka kutokana na tatizo hilo na ikisiwa ifikapo 2050 jumla ya watu 10 milioni watakufa kwa mwaka.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mhe.Anthony Mavunde akihitimisha kampeni ya Elimu ya Tatizo la Usugu wa vimelea vya dawa katika Shule ya Sekondari ya Wasichana-Msalato,Dodoma

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mhe.Anthony Mavunde akiwa na wanafunzi wa shule ya Wasichana Msalato katika kampeni ya Elimu ya Tatizo la Usugu wa vimelea vya dawa.

Chama cha Wanafunzi Wafamasia Tanzania(TASPA) wakiwa katika uhitimishaji wa kampeni ya Elimu ya Tatizo la Usugu wa vimelea vya dawa katika Shule ya Sekondari ya Wasichana-Msalato,Dodoma

Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Wasichana Msalato wakiwa katika kampeni ya Elimu ya Tatizo la Usugu wa vimelea vya dawa katika Shule ya Sekondari ya Wasichana-Msalato,Dodoma

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mhe.Anthony Mavunde akipanda mti katika Shule ya Sekondari ya Wasichana-Msalato,Dodoma



Hivyo makala MAVUNDE ASISITIZA ELIMU ZAIDI JUU YA TATIZO LA USUGU WA VIMELEA VYA DAWA

yaani makala yote MAVUNDE ASISITIZA ELIMU ZAIDI JUU YA TATIZO LA USUGU WA VIMELEA VYA DAWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAVUNDE ASISITIZA ELIMU ZAIDI JUU YA TATIZO LA USUGU WA VIMELEA VYA DAWA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/mavunde-asisitiza-elimu-zaidi-juu-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MAVUNDE ASISITIZA ELIMU ZAIDI JUU YA TATIZO LA USUGU WA VIMELEA VYA DAWA"

Post a Comment

Loading...