Loading...

MKAPA AONGOZA HARAMBEE KUCHANGIA MFUKO WA UDHAMINI KUDHIBITI UKIMWI

Loading...
MKAPA AONGOZA HARAMBEE KUCHANGIA MFUKO WA UDHAMINI KUDHIBITI UKIMWI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MKAPA AONGOZA HARAMBEE KUCHANGIA MFUKO WA UDHAMINI KUDHIBITI UKIMWI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MKAPA AONGOZA HARAMBEE KUCHANGIA MFUKO WA UDHAMINI KUDHIBITI UKIMWI
link : MKAPA AONGOZA HARAMBEE KUCHANGIA MFUKO WA UDHAMINI KUDHIBITI UKIMWI

soma pia


MKAPA AONGOZA HARAMBEE KUCHANGIA MFUKO WA UDHAMINI KUDHIBITI UKIMWI

Na Dotto Mwaibale

RAIS Mstaafu Benjamin Mkapa amewataka wadau mbalimbali na wananchi kuendelea kuchangia Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi (ATF) kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa huo nchini ambapo zaidi ya sh.milioni 200 zilipatikana.

Mkapa alitoa ombi hilo wakati akiongoza harambee ya kuchangia mfuko huo iliyofanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali, wawakilishi wa mashirika ya nje na ndani pamoja na mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini.

"Ni wajibu kwa kila mwananchi na wadau mbalimbali kuendelea kuchangia mfuko huu ili kusaidia mapambano ya Ukimwi hapa nchini na kuwa mapmbano hayo si ya mtu mmoja" alisema Mkapa. Katika hatua nyingine Rais Mstaafu Mkapa ameiomba Serikali kuendelea kutenga fedha za Ukimwi katika bajeti zake.

Akizungumza katika harambee hiyo Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mheshimiwa Jenista Mhagama alisema kwamba Serikali itaendelea kusimamia Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) katika matumizi ya fedha hizo.

Mhagama alisema asilimia 60 ya fedha hizo zitatumika kununulia madawa, asilimia 25 itatumika katika kutoa huduma za kinga pamoja na kutoa elimu ya kujikinga na maambukizi mapya ya Ukimwi na asilimia 15 zitatumika kwa ajili ya uwezeshaji na ufuatiliaji wa programu za Ukimwi.
Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa akitoa zawadi ya picha iliyonunuliwa kwa sh. milioni moja katika harambee hiyo.
Rais Mkapa akimkabidhi picha Salama Mussa kutoka Benki ya NBC baada ya kuinunua katika harambee hiyo. Kulia ni Waziri Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mheshimiwa Jenista Mhagama na wa pili kushoto ni Mdau Teddy Mapunda mratibu wa harambee hiyo.
Rais Mstaafu, Benjamini Mkapa akimkabidhi picha Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Alvaro Rodriguez baada ya kuinunua katika harambee hiyo.
Rais Mstaafu, Benjamini Mkapa akimkabidhi picha ya simba Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa Hoteli ya Serena, Bw. Seraphin Lusala baada ya kuinunua kwenye harambee hiyo.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Geita Gold Mine (GGM), Bw. Tenga B. Tenga akimkabidhi Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa mfano wa hundi yenye thamani ya sh.milioni 100 zilizo tolewa na mgodi huo kuchangia mfuko huo.





Hivyo makala MKAPA AONGOZA HARAMBEE KUCHANGIA MFUKO WA UDHAMINI KUDHIBITI UKIMWI

yaani makala yote MKAPA AONGOZA HARAMBEE KUCHANGIA MFUKO WA UDHAMINI KUDHIBITI UKIMWI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MKAPA AONGOZA HARAMBEE KUCHANGIA MFUKO WA UDHAMINI KUDHIBITI UKIMWI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/mkapa-aongoza-harambee-kuchangia-mfuko.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MKAPA AONGOZA HARAMBEE KUCHANGIA MFUKO WA UDHAMINI KUDHIBITI UKIMWI"

Post a Comment

Loading...