Loading...
title : MTOTO AUWAWA KIKATILI MKOANI MTWARA
link : MTOTO AUWAWA KIKATILI MKOANI MTWARA
MTOTO AUWAWA KIKATILI MKOANI MTWARA
Mtoto mwenye umri wa miaka Mitano Jazaka Mussa, ameuwawa kikatili kwa kukatwa na Panga kichwani na mtu asiyefahamika katika kijiji cha Lipwidi, halmashauri ya wilaya ya Mtwara.
Akithibitisha taarifa za tukio hilo, kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara, Lucas Mkondya, amesema muuwaji alimvamia mama wa mtoto huyo, Amina Saidi ambae alimbeba mwanae mgongoni na kumkaba huku akimlazimisha awe mke wake, kabla ya mama huyo kumdondosha mtoto na kukimbia.
Aidha, kamanda huyo wa Polisi ameongeza kuwa, baada ya tukio hilo, wananchi wenye hasira kali walifika eneo la tukio na kisha kumshambulia mpaka kufa muuwaji huyo na kisha kumchoma moto.
Jeshi la Polisi bado linaendelea na upelelezi wa tukio hilo ili kujua undani wake, ambapo bado muuwaji hajafahamika kwa majina na makazi yake.
Hivyo makala MTOTO AUWAWA KIKATILI MKOANI MTWARA
yaani makala yote MTOTO AUWAWA KIKATILI MKOANI MTWARA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MTOTO AUWAWA KIKATILI MKOANI MTWARA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/mtoto-auwawa-kikatili-mkoani-mtwara.html
0 Response to "MTOTO AUWAWA KIKATILI MKOANI MTWARA"
Post a Comment