Loading...
title : MTULIA ASEMA SHIDA ZA WANANCHI KINONDONI NI ZAKE, ATAJA ATAKAYOANZA NAYO AKIWA MBUNGE
link : MTULIA ASEMA SHIDA ZA WANANCHI KINONDONI NI ZAKE, ATAJA ATAKAYOANZA NAYO AKIWA MBUNGE
MTULIA ASEMA SHIDA ZA WANANCHI KINONDONI NI ZAKE, ATAJA ATAKAYOANZA NAYO AKIWA MBUNGE
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii
MGOMBEA ubunge jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Abdallah Mtulia ameendelea kuomba kura huku akiwaambi wananchi yeye hana tofauti na wao.
Pia shida za wananchi ni shida zake, matatizo yao ni matatizo yake pia na kuongeza yeye in mtoto wa kimaskini.tulia amesema hayo kwa nyakati tofauti kwenye mikutano yake ya kampeni kwenye uchaguzi huo wa jimbo hilo.Hata hivyo wakati Mtulia akiomba kura kwa wananchi hao wa Kinondoni, mgombea ubunge wa Chadema Salum Mwalimu naye ameendelea kuomba kura.
Mwalimu amekuwa akitoa Sera mbalimbali zenye lengo kuleta maendeleo kwa wananchi wa jimbo na kwamba anaamini yeye ndio mgombea sahihi ,hivyo wamchague alete maendeleo.Wakati wagombea hao kila mmoja akiomba kura za wananchi hao ,kwa Mtulia yeye ameendelea kusisitiza changamoto za jimbo hilo anazijua na anao uwezo wa kuzitatua.
"Niliguswa na matatizo yenu ya kubomolewa nyumba nikaenda Mahakamani kuzuia bomoabomoa nikafanikiwa."Nilipambana kuhakikisha watu waliobomolewa wanapata hifadhi Magomeni. Nimekuja CCM kuhakikisha hilo linatimia," amesema Mtulia. Ameongeza kuwa "Niliacha ubunge, mshahara, posho na kiinua mgongo changu kwa sababu nawajali wana Kinondoni. Ukiwa jiongozi wa upinzani hauwezi kufanya lolote.
"Maendeleo hayapatikani kwa kutukana, kukashifu, matusi. Maendeleo huja kwa ushirikiano na mahusiano mema," amesema.Amefafanua zaidi ni kweli anampenda Rais,Dk.John Magufuli na kuuliza ataachaje Rais ambaye anajenga reli ya kisasa, kununua ndege za kisasa, ujenzi wa mradi mkubwa wa umeme. Rais mkweli na muwazi.
MGOMBEA ubunge jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Abdallah Mtulia ameendelea kuomba kura huku akiwaambi wananchi yeye hana tofauti na wao.
Mbunge wa jimbo la Mtera,Livingstone Lusinde akimnadi Mgombea Ubunge jimbo la Kinondoni jana jioni katika viwanja vya Vegas,Makumbusho,Kinondoni jijini Dar.
Baadhi ya Wananchi na wafuasi wa chama cha CCM wakiwa wamekusanyika kwenye kampeni katika viwanja vya Vegas,Makumbusho Kinondoni jijini Dar
Hivyo makala MTULIA ASEMA SHIDA ZA WANANCHI KINONDONI NI ZAKE, ATAJA ATAKAYOANZA NAYO AKIWA MBUNGE
yaani makala yote MTULIA ASEMA SHIDA ZA WANANCHI KINONDONI NI ZAKE, ATAJA ATAKAYOANZA NAYO AKIWA MBUNGE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MTULIA ASEMA SHIDA ZA WANANCHI KINONDONI NI ZAKE, ATAJA ATAKAYOANZA NAYO AKIWA MBUNGE mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/mtulia-asema-shida-za-wananchi.html
0 Response to "MTULIA ASEMA SHIDA ZA WANANCHI KINONDONI NI ZAKE, ATAJA ATAKAYOANZA NAYO AKIWA MBUNGE"
Post a Comment