Loading...
title : Mtumishi wa CCM Zanzibar afariki dunia
link : Mtumishi wa CCM Zanzibar afariki dunia
Mtumishi wa CCM Zanzibar afariki dunia
SALAMU ZA RAMBI RAMBI
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dk. Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’ ametuma salamu za rambi rambi kwa familia ya Mtumishi wa Chama Marehemu Bw. Maulid Sleyum Said aliyefariki Februari 16 ,2018.
Bw.Maulid amefariki dunia akiwa katika hospitali ya Global iliyopo Vuga Mjini Zanzibar alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kuugua ghafla.
Katika Salamu zake Dk. Mabodi amesema CCM imepokea taarifa ya kifo cha mtumishi huyo kwa Mshutuko, Majonzi na uzuni kubwa, kwani Marehemu enzi za uhai wake alikuwa Mwadilifu aliyefanya kazi kwa bidii katika utumishi wake kwa muda wote wa uhai wake.
Pamoja na hayo ametoa pole kwa Wanachama, Viongozi na Watendaji Wote wa CCM Zanzibar na Tanzania kwa ujumla, Marafiki pamoja na Ndugu na Jamaa wa karibu walioguswa na msiba, na kuwaomba waendelee kuwa na uvumilivu katika kipindi chote cha msiba huu.
Pia ameiomba Familia ya Marehemu kuwa na Subra katika kipindi hiki kigumu cha Msiba huu, huku wakiendelea kumuombea dua.
Enzi za uhai wake Marehemu Bw.Maulid Sleyum amefanya kazi katika Afisi Kuu CCM Zanzibar kwa nafasi ya uhudumu.
Marehemu atazikwa kesho kijijini kwao Zingwezingwe Wilaya ya Kaskazini ‘’B” Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Bw. Maulid Sleyum amezaliwa mwaka 1960 na ameacha kizuka mmoja na watoto watatu.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu pahala Pema Peponi Amin.
Hivyo makala Mtumishi wa CCM Zanzibar afariki dunia
yaani makala yote Mtumishi wa CCM Zanzibar afariki dunia Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mtumishi wa CCM Zanzibar afariki dunia mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/mtumishi-wa-ccm-zanzibar-afariki-dunia.html
0 Response to "Mtumishi wa CCM Zanzibar afariki dunia"
Post a Comment