Loading...
title : TANESCO YAFANYA MSAKO WEZI WA UMEME
link : TANESCO YAFANYA MSAKO WEZI WA UMEME
TANESCO YAFANYA MSAKO WEZI WA UMEME
Shirika la Umeme Tanzania TANESCO Kupitia kikosi kazi maalum limeendesha kampeni kabambe ya kubaini na kutokomeza matukio ya wizi wa umeme pamoja na uhujumu miundombinu ya Shirika Mkoani Njombe ikiwa ni mwendelezo wa jitihada endelevu za TANESCO katika kudhibiti upotevu wa mapato ya Shirika.
Akiongea katika kampeni hiyo, Kaimu Meneja wa TANESCO Makao Makuu anayesimamia Wateja Wakubwa Mhandisi Fredrick Njavike ambaye pia ameongoza Zoezi hilo alisema kuwa, ndani ya siku tano kupitia kampeni hiyo tayari wamekagua takribani wateja 2000 katika Wilaya ya makambako pekee huku Njombe Mjini wakitarajia kukagua wateja 1000.
Njavike ameongeza kuwa katika idadi ya wateja waliokaguliwa, wateja kadhaa walibainika kujihusisha na vitendo vya wizi wa Umeme. Kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama Mkoa wa Njombe wahalifu hao walichukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kulipa gharama za kiasi chote cha umeme walichokuwa wakiliibia Shirika baada ya kupigiwa mahesabu.
"Zoezi hili la ukaguzi na msako wa wezi wa umeme ni zoezi endelevu linalofanyika Nchi nzima na niwatahadharishe wale wote wanaojihusisha na vitendo hivyo kuacha mara moja, kwani ni lazma watagundulika na hatua kali za kisheria dhidi yao zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na malipo ya fidia ya kiasi cha umeme walicholiibia Shirika.
Hivyo niwaombe Wananchi kuendelea kutupa ushirikiano kwa kufichua watu wenye viashiria vya Wizi wa Umeme. Lakini pia niwaombe wateja wetu kutoa taarifa TANESCO pale wanapona hitilafu zozote katika mita zao pamoja na kuepukana na vishoka wanaowashawishi waibe umeme kwani kupitia msako huu hakuna atakayeiba Umeme na akasalimika bila kukuamatwa na kuchukuliwa hatua" Alisema Mhandisi Njavike
Naye Meneja wa TANESCO Mkoa wa Njombe, Mhandisi Emmanuel Kachewa ametoa Wito kwa Wananchi wa Mkoa wa Njombe kuendelea kushirikiana na TANESCO katika kuwafichua wezi wa Umeme popote walipo ili waweze kuchukuliwa hatua na kuokoa upotevu wa mapato ya Shirika kwa ujumla.
Kwa upande wa baadhi ya wananchi walioshuhudia msako huu ukifanyika mitaani waliipongeza TANESCO kwa kuanza kutambua thamani ya mali zao na kulinda umeme wao ambapo mwanchi mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Mponzi alisema kuwa Matukio ya wizi wa umeme yapo mtaani na wakati mwingine yamekuwa yakisababisha hata vifo kwa wahusika kunaswa na umeme wakati wakijaribu kuiba umeme hivyo ni vyema TANESCO pia Wakatoa na Elimu juu ya madhara ya Wizi wa umeme kwa wananchi wote wafahamu.
Aidha TANESCO imekuwa ikiingia hasara kutokana na vitendo vya wateja wachache ambao kwa makusudi kabisa wamekuwa wakiliibia Shirika umeme kwa katika maeneo mbalimbali na hivyo kulikosesha Shirika mapato stahiki na kurudisha nyuma jitihada za TANESCO na Serikali Katika kusambaza Umeme Nchi nzima na hivyo kufifisha kasi ya Uimarishaji wa Miundombinu ya Uzalishaji, Ufuaji na Usambazaji umeme Nchini.
Hivyo makala TANESCO YAFANYA MSAKO WEZI WA UMEME
yaani makala yote TANESCO YAFANYA MSAKO WEZI WA UMEME Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TANESCO YAFANYA MSAKO WEZI WA UMEME mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/tanesco-yafanya-msako-wezi-wa-umeme.html
0 Response to "TANESCO YAFANYA MSAKO WEZI WA UMEME"
Post a Comment