Loading...
title : TTCL WAZINDUA HUDUMA MPYA YA FIBER CONNECT BUNDLE
link : TTCL WAZINDUA HUDUMA MPYA YA FIBER CONNECT BUNDLE
TTCL WAZINDUA HUDUMA MPYA YA FIBER CONNECT BUNDLE
MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL CORPORATION) Waziri Kindamba ametangaza uzinduzi wa huduma mpya iliyopewa jina la Fiber Connect Bundle huku akitumia kauli mbiu yao inayosema Rudi nyumbani, kumenoga.
Amefafanua huduma hiyo mpya ambayo wameizindua leo jijini Dar es Salaam ni mwendelezo wa ubunifu wa kampuni hiyo ya kizalendo katika kuwapatia watanzania huduma za kipekee na zenye ubora wa hali ya juu. Kindamba amesema TTCL Corporation imechukua hatua kwa kuwafuata wateja nyumbani na kufanya mapinduzi makubwa ya kimawasiliano hasa ya mtandao wa intanenti yenye kasi balaa.
Amesema kupitia huduma hiyo mpya ya Fiber Connect Bundle, wateja wao watapata huduma nne kwa pamoja zikiwa na unafuu mkubwa wa gharama na ubora wa hali ya juu ukilinganisha na kwa majirani zao. Kindamba amefafanua huduma kwa kuanzia wanatarajia kuzifikia nyumba 500 katika maeneo ya Mikocheni na nyumba nyingine 500 katika eneo la Mbezi Beach jijini Dar es Salaam pamoja na nyumba 200 eneo la Medeli mkoani Dodoma.
Amesema baada ya hapo wataendelea na maeneo mengine kwani lengo lao ni kuhakikisha kila mahali katika nchi yetu kunakuwa na huduma za mawasiliano ya Shirika hilo hasa kwa kuzingatia wao ndio wanaousimamia mkongo wa Taifa wa mawasilano. Kindamba amesema kupitia kifurushi cha Fiber Connect, mteja wao atanufaika na huduma mbalimbali ikiwamo ya kupata intanenti yenye kasi isiyo na kikomo (Unlimited)
Pia mteja atapata huduma ya simu za sauti kwa simu za mezani na simu card ambayo ataitumia kwenye simu yake ya mkononi na kupata huduma ya Intanenti sawa na simu ile anayopata katika simu ya mezani. Ameongeza kuwa mteja wao pia atapata huduma za Wireless Service (WIFI) katika nyumba yake ambapo vifaa vyote vinavyotumia teknolojia ya intaneti vitaunganishwa ili kutumia kutumia huduma hiyo.
Ametoa mfano kuwa huduma ambayo wameizundua mteja anaweza kuunganisha kwenye Smart Tv, Tablets na kompyuta mpakato.Pia mteja atapatiwa vifaa vyote bure na uhakika wa huduma za baada (After Sell Services) endapo itahitajika. Kindamba amesema kuwa wamejipanga kuhakikisha wanaendelea kutoa huduma bora kwa ajili ya Watanzania ambao kimsingi shirika hilo ni mali yao na wanatakiwa kuunga mkono jitihada hizo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania(TTCL Corporation),Waziri Kindamba akizungumza leo jijini Dar es Salaam kuhusu huduma mpya ambayo wameizindua inayojulikana Fiber Connect yenye kasi balaa ya intanent kwa ajili ya wateja wao.
Hivyo makala TTCL WAZINDUA HUDUMA MPYA YA FIBER CONNECT BUNDLE
yaani makala yote TTCL WAZINDUA HUDUMA MPYA YA FIBER CONNECT BUNDLE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TTCL WAZINDUA HUDUMA MPYA YA FIBER CONNECT BUNDLE mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/ttcl-wazindua-huduma-mpya-ya-fiber.html
0 Response to "TTCL WAZINDUA HUDUMA MPYA YA FIBER CONNECT BUNDLE"
Post a Comment