Loading...

UGENI MAHAKAMA YA JUU NCHINI GUATEMALA WAKUTANA NA JAJI MKUU WA TANZANIA

Loading...
UGENI MAHAKAMA YA JUU NCHINI GUATEMALA WAKUTANA NA JAJI MKUU WA TANZANIA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa UGENI MAHAKAMA YA JUU NCHINI GUATEMALA WAKUTANA NA JAJI MKUU WA TANZANIA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : UGENI MAHAKAMA YA JUU NCHINI GUATEMALA WAKUTANA NA JAJI MKUU WA TANZANIA
link : UGENI MAHAKAMA YA JUU NCHINI GUATEMALA WAKUTANA NA JAJI MKUU WA TANZANIA

soma pia


UGENI MAHAKAMA YA JUU NCHINI GUATEMALA WAKUTANA NA JAJI MKUU WA TANZANIA

Na Mary Gwera

Katika mwendelezo wa Utekelezaji wa Mpango Mkakati wake wa miaka mitano (5) (2015/2016-2019/2020), Mahakama ya Tanzania inaendelea na jitihada za kupata uzoefu na ujuzi kutoka katika Mahakama mbalimbali duniani zilizopiga hatua katika maboresho ya huduma ya utoaji haki kwa wananchi.

Haya yamejidhihirisha kufuatia ugeni wa Maafisa wa Mahakama waliowasili kutoka nchini Guatemala kwa mualiko wa Mahakama ya Tanzania kushiriki katika Hafla ya Siku ya Sheria nchini, iliyofanyika Februari 01, 2018 vilevile Mahakama ya Tanzania kupata maoni na ushauri zaidi wa jinsi ya kuendelea kuiboresha Mahakama nchini kwa manufaa ya wananchi ambao ndio walengwa Wakuu.

Akiwatambulisha wageni hao kwa Mhe. Jaji Mkuu wa Tanzania, Februari 1 katika Ofisi ya Mhe. Jaji Mkuu, Mahakama ya Rufani Dar es Salaam, Mtendaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga alisema kuwa takribani miaka mitatu sasa baadhi ya Maafisa wa Mahakama nchini walifanya ziara nchini Guatemala kwa lengo la kujifunza ni kwa namna gani Mahakama nchini Guatemala imefanikiwa katika utoaji wa huduma zake.

“Mhe. Jaji Mkuu, tulichojifunza na tukaona ni vyema kuiga kutoka Guatemala ni pamoja na huduma ya Mahakama inayotembea ‘mobile court’, ufanyaji kazi wa Mahakama kwa masaa 24, kuweka mbele matumizi ya teknolojia katika shughuli zake  n.k, hivyo tumeona ni vyema pia kwa Mahakama nchini kupata utaalamu/uzoefu kutoka kwa wenzetu jinsi ya kuweza kutekeleza haya,” alisema Bw. Kattanga.
  Jaji Mkuu wa Tanzania (pichani) akiwa katika mazungumzo na Wageni hao (hawapo pichani), katika mazungumzo yao Mhe. Jaji Mkuu amefurahishwa na hatua iliyofikiwa na Mahakama nchini Guatemala.
 Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali akiongea jambo na Wageni hao, Mhe. Wambali aliwaelezea Wageni hao juu ya Mfumo wa Mahakama nchini.
  Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (aliyeketi mbele) akiwa pamoja na baadhi ya Wahe. Majaji wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Jaji Kiongozi, Mtendaji Mkuu na Ugeni kutoka Mahakama nchini Guatemala pindi Wageni hao walipomtembelea Mhe. Jaji Mkuu ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
 Jaji Mkuu aliyemaliza muda wake wa Mahakama nchini Guatemala, Mhe. Osvaldo Mendez akizungumza jambo.
 Mtaalamu kutoka Benki ya Dunia, Bw. Waleed Malik akiongea jambo katika kikao hicho.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala UGENI MAHAKAMA YA JUU NCHINI GUATEMALA WAKUTANA NA JAJI MKUU WA TANZANIA

yaani makala yote UGENI MAHAKAMA YA JUU NCHINI GUATEMALA WAKUTANA NA JAJI MKUU WA TANZANIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala UGENI MAHAKAMA YA JUU NCHINI GUATEMALA WAKUTANA NA JAJI MKUU WA TANZANIA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/ugeni-mahakama-ya-juu-nchini-guatemala.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "UGENI MAHAKAMA YA JUU NCHINI GUATEMALA WAKUTANA NA JAJI MKUU WA TANZANIA"

Post a Comment

Loading...