Loading...
title : WAZIRI MAHIGA AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA MABALOZI WA VIETNAM NA JAPAN WALIOPO NCHINI
link : WAZIRI MAHIGA AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA MABALOZI WA VIETNAM NA JAPAN WALIOPO NCHINI
WAZIRI MAHIGA AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA MABALOZI WA VIETNAM NA JAPAN WALIOPO NCHINI
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Balozi wa Vietnam nchini, Mhe. Kim Nguyen Doanh. Katika mazungumzo yao walisisitiza umuhimu wa kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizi mbili hususan katika masuala ya biashara na uwekezaji.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Justa Nyange (kushoto) pamoja na Bw. Emmanuel Luangisa (katikati), Afisa Mambo ya Nje na Bw. Magabilo Murobi (kulia), Katibu wa Waziri wakifuatilia mazungumzo kati ya Mhe. Mahiga na Mhe. Kim Nguyen Doanh (hawapo pichani)
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Balozi wa Japan nchini, Mhe. Masaharu Yoshida. Mazungumzo yao yalijikita kwenye kuimarisha ushirikiano katika masuala mbalimbali ya manufaa kwa nchi hizi mbili.
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Celestine Mushy akifafanua jambo wakati wa mazungumzo kati ya Mhe. Mahiga na Balozi wa Japan nchini, Mhe. Yoshida (hawapo pichani). Wengine katika picha ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Justa Nyange (kushoto) Bw. Abdallah Kirungu (katikati), Afisa Mambo ya Nje na Bw. Magabilo Murobi (kulia), Katibu wa Waziri.
Hivyo makala WAZIRI MAHIGA AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA MABALOZI WA VIETNAM NA JAPAN WALIOPO NCHINI
yaani makala yote WAZIRI MAHIGA AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA MABALOZI WA VIETNAM NA JAPAN WALIOPO NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MAHIGA AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA MABALOZI WA VIETNAM NA JAPAN WALIOPO NCHINI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/waziri-mahiga-akutana-kwa-mazungumzo-na.html
0 Response to "WAZIRI MAHIGA AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA MABALOZI WA VIETNAM NA JAPAN WALIOPO NCHINI"
Post a Comment