Loading...

AIRTEL YAZINDUA BANDO LA YATOSHA MITANDANO YOTE

Loading...
AIRTEL YAZINDUA BANDO LA YATOSHA MITANDANO YOTE - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa AIRTEL YAZINDUA BANDO LA YATOSHA MITANDANO YOTE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : AIRTEL YAZINDUA BANDO LA YATOSHA MITANDANO YOTE
link : AIRTEL YAZINDUA BANDO LA YATOSHA MITANDANO YOTE

soma pia


AIRTEL YAZINDUA BANDO LA YATOSHA MITANDANO YOTE



Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania inayoongoza kwa kutoa huduma bora za smartphone leo imetangaza uhuru wa mawasiliano kwa kuzindua huduma kabambe ya kipekee kwa wateja wake wanaopiga simu na kutuma sms kwenda mitandao yote nchini. 

Taarifa iliyotolewa na Airtel leo imesema bando za uhuru zinakuja baada ya serikali hivi karibuni kuweka punguzo kubwa la gharama za kuunganisha simu zinazokwenda mitandao mingine (interconnection rate) na hivyo Airtel kuona vyema kuwapa wateja wake fursa ya kufurahia punguzo hilo kupitia huduma yake itakayojulikana kama ‘Yatosha Mitandao Yote’. Wateja wote watapiga na kutuma sms mtandao wowote nchini baada ya kujinunulia bando nafuu ya shilingi 1000 au bando mpya ya shilingi 600 tu.

 ‘Yatosha Mitandao Yote’ ni bando bora kuliko zote nchini zinazowawezesha wateja wa Airtel kujipatia vifurushi vyenye muda wa maongezi mara mbili zaidi ya  ilivyokuwa awali. Mteja atapata dakika 50, 10MB za intaneti na sms za bure 50 kwenda mitandao yote kwa shilingi 1000 tu kwa saa 24, hapo awali kifurushi hiki cha shilingi 1000 mteja alipata dakika 25 tu. 

Vilevile kwa kifurushi kipya kimeongezwa faida ili kumpa mteja dakika 16, 2MB na 50 sms  kwenda mitando yote kwa shilingi 600 tu. Zaidi ya hapo wataendelea kujipatia vifurushi nafuu kwa SIKU, WIKI, MWEZI kwa kujiunga baada ya kununua vocha kwa kupiga *149*99# kisha chagua YATOSHA MITANDAO YOTE au kujiunga kupitia huduma ya Airtel Money na kufurahia Uhuru wa kuongea.

Akiongea jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzindua wa Yatosha Mitandao Yote, Mkurugenzi Mtendaji Airtel Tanzania Sunil Colaso alisema kuwa “wateja wanabaki kuwa ndio nguzo kuu yetu kwenye biashara, ni furaha kubwa kwetu kuzindua huduma ya Yatosha Mitandao Yote ambayo itawapa wateja wa Airtel unafuu zaidi na uhuru  wa kutumia huduma za mawasiliano. Tunaendelea kufanya utafiti kufahamu mahitaji ya wateja pamoja na kuongeza ubunifu ili kuleta huduma nafuu zaidi ”

“Tunaipongeza serikali yetu kwa kupunguza gharama za kuunganisha simu mitandao mingine kutoka Shilingi 26.96 kwa dakika hadi shilingi 15.6 kwa dakika kuanzia januari, Airtel tunaona fahari sana kuwapa wateja wetu unafuu huo kupitia huduma yetu ya Yatosha Mitandao Yote. Mteja anatakiwa kuwa tu na laini iliyosajiliwa ya Airtel ili kufurahia huduma zetu bora na nafuu” aliezeza Colaso 

Yatosha Mitandao Yote inawafanya wateja kufurahi na kufanya mipango ambayo inayoendana na hali ya maisha na kutoa Uhuru wa kuunganisha familia, marafiki na wanafanya biashara kupitia mtandao wa Airtel kwenye mitandao mingine nchini kote na kwa muda wowote.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano alisema kuwa “Airtel tumeboresha upya huduma ya Yatosha bando ili kuongeza muda wa mangezi na kupanua uhuru  kwa  kutoa fursa kwa wateja kutumia huduma ya Yatosha Mitando Yote kwa kutuma sms, kupinga simu kwenda mitandao yote kwa kuanzia shilingi 600 tu. Ukiwa na Airtel Yatosha mahitaji yako ya mawasiliano yametimia!

“Kwa kujiunga na Yatosha Mitando Yote, wateja watatakiwa kupinga *149*99# halafu changua 3 ili kununua bando ya ‘Yatosha Mitandao Yote’ kulingana na mahitaji yako. Tuna uhakika kuwa huduma ya Yatosha Mitandao Yote itarahisisha maisha” alisisitiza Bi Singano

Yatosha Mitandao Yote ni moja ya bidhaa za Airtel Yatosha, Airtel hivi karibuni pia ilizindua bando za intaneti za Yatosha SMATIKA Intaneti ambayo inatoa 2GB kwa Tzs 2000 ambazo zinadumu kwa siku 3. Wateja wa Airtel wanaojiunga na Smatika bando wanajishindia simu mpya za smartphone, modem na 1GB kwa wateja 1000 kila siku.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya simu za mkononi Airtel Tanzania Sunil Colaso akiongea na waandishi wa habari baada ya uzinduzi bando za Uhuru zaidi inayojulikana kama ‘Yatosha Mitandao Yote’. Kwa Yatosha Mitandao Yote mteja atapata dakika 50, 10MB za intaneti na sms za bure 50 kwenda mitandao yote kwa shilingi 1000 tu kwa saa 24. Kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano Beatrice Singano na kushoto Afisa Mkuu wa Biashara Rohit Tandon.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya simu za mkononi Airtel Tanzania, Sunil Colaso(katikati), Mkurugenzi wa Mawasiliano, Beatrice Singano(kulia) na kushoto Afisa Mkuu wa Biashara Rohit Tandon, wakionyesha bango baada ya kuzindua bando za Uhuru zaidi inayojulikana kama ‘Yatosha Mitandao Yote’. Kwa Yatosha Mitandao Yote mteja atapata dakika 50, 10MB za intaneti na sms za bure 50 kwenda mitandao yote kwa shilingi 1000 tu kwa saa 24.

Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania, Beatrice Singano akiongea na waandishi wa habari baada ya uzinduzi bando za Uhuru zaidi inayojulikana kama ‘Yatosha Mitandao Yote’. Kwa Yatosha Mitandao Yote mteja atapata dakika 50, 10MB za intaneti na sms za bure 50 kwenda mitandao yote kwa shilingi 1000 tu kwa saa 24. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Sunil Colaso.



Hivyo makala AIRTEL YAZINDUA BANDO LA YATOSHA MITANDANO YOTE

yaani makala yote AIRTEL YAZINDUA BANDO LA YATOSHA MITANDANO YOTE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala AIRTEL YAZINDUA BANDO LA YATOSHA MITANDANO YOTE mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/03/airtel-yazindua-bando-la-yatosha.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "AIRTEL YAZINDUA BANDO LA YATOSHA MITANDANO YOTE"

Post a Comment

Loading...