Loading...
title : ATAKAYEHUJUMU UJENZI WA MRADI WA MAJI TOKA ZIWA VICTORIA KUKIONA - RC MWANRI
link : ATAKAYEHUJUMU UJENZI WA MRADI WA MAJI TOKA ZIWA VICTORIA KUKIONA - RC MWANRI
ATAKAYEHUJUMU UJENZI WA MRADI WA MAJI TOKA ZIWA VICTORIA KUKIONA - RC MWANRI
SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imesema itamchukulia hatua kali mtu yoyote atakayebainika kuhujumu utekelezaji wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda Mkoani humo wenye gharama ya bilioni 600 kwa ajili ya kusaidia kutoa huduma ya maji safi na salama kwa wakazi wa eneo hilo.
Kauli hiyo imetolewa leo wilayani Nzega na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wakati alipotembelea na kukagua mradi huo unaotoa maji katika Kijiji cha Solwa mkoani Shinyanga kupeleka mkoani Tabora ambapo wilaya za Nzega, Igunga, Uyui na Tabora mjini zitanufaika na mradi huo wa maji kutoka ziwa Victoria unaotekelezwa kwa muda wa miezi thelathini.
Alisema kuwa Serikali haitamfumbia macho mtu yeyote atakayebainika kuwa na nia ovu ya kutaka kuiba vifaa mbalimbali ambavyo vinatumiwa na wakandarasi katika kujenga mradi huo ambao ni muhimu sana kwa ajili ya wakazi wa maeneo mbali ya Tabora.
Mwanri alisema kuwa hadi sasa kazi inaendelea ambapo Mkandarasi ya kampuni ya L & T yupo kazini akiendelea na shughuli ya kuunga na kufukia mabomba ardhini na kueleza kuwa hujuma yoyote ambayo inaweza kujitokeza inaaweza kusababisha mradi kuchelewa kumalizika kusababisha wakazi wa maeneo ambao yalikuwa yapate huduma hiyo kuendelea kupata matatizo ya maji.
Alisema kuwa kama kuna matatizo yoyote wanayopata kama vile wizi wa vifaa ni vema wakaeleza ili uongozi wa Mkoa uweze kuchukua hatua mapema kwa ajili ya kuendelea kuwawekea mazingira mazuri ya ujenzi wa mradi huo na kuongeza kuwa kama watapata matatizo na kunyamaza na muda wa kukamilisha mradi utafika wakiwa bado hawajakamilisha Serikali haitasikiliza.
Mwanri aliwataka Wakuu wote wa Wilaya na Watendaji wote ambapo mradi huo unapita kuhakikisha wanasimamia ili isije ikatokee hujuma yoyote na kama ilitokea wakamate watu wote wanatuhumiwa.
Naye Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Mkama Bwire alisema kuwa utekelezaji wa mradi huo upo ndani ya utekelezaji na tayari hata malipo ya fidia kwa wananchi waliopitiwa maeneo yao na mradi yamekwishafanyika. Alisema wananchi 204 ambao maeneo yanapitiwa na Mradi huo na kukabainika kuwa wanatarajiwa kulipwa milioni 890.5 zitatumika kama fidia kwa wananchi hao
Alisema kuwa jumla ya milioni 760 zimeshalipwa kwa wananchi zaidi ya 162 ambao maeneo yao yalikwishafanyiwa tathmini.
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Nzega alisema wananchi wa wilaya yake wanaupokea Mradi huo kwa furaha kwa kukamilika kwake kutasaidia kuwaondolea tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama ya uhakika. Mradi huu wa Maji unatarajia kuwanufaisha wakazi wa Mkoa wa Tabora wapatao milioni moja ambao watakuwa na uhakika wa maji safi na salama.
Hivyo makala ATAKAYEHUJUMU UJENZI WA MRADI WA MAJI TOKA ZIWA VICTORIA KUKIONA - RC MWANRI
yaani makala yote ATAKAYEHUJUMU UJENZI WA MRADI WA MAJI TOKA ZIWA VICTORIA KUKIONA - RC MWANRI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ATAKAYEHUJUMU UJENZI WA MRADI WA MAJI TOKA ZIWA VICTORIA KUKIONA - RC MWANRI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/03/atakayehujumu-ujenzi-wa-mradi-wa-maji.html
0 Response to "ATAKAYEHUJUMU UJENZI WA MRADI WA MAJI TOKA ZIWA VICTORIA KUKIONA - RC MWANRI"
Post a Comment