Loading...

CCM ZANZIBAR YATOA AGIZO ZITO KWA VIONGOZI WA CHAMA NA SERIKALI

Loading...
CCM ZANZIBAR YATOA AGIZO ZITO KWA VIONGOZI WA CHAMA NA SERIKALI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa CCM ZANZIBAR YATOA AGIZO ZITO KWA VIONGOZI WA CHAMA NA SERIKALI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : CCM ZANZIBAR YATOA AGIZO ZITO KWA VIONGOZI WA CHAMA NA SERIKALI
link : CCM ZANZIBAR YATOA AGIZO ZITO KWA VIONGOZI WA CHAMA NA SERIKALI

soma pia


CCM ZANZIBAR YATOA AGIZO ZITO KWA VIONGOZI WA CHAMA NA SERIKALI

NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
TASNIA ya Habari ni sekta muhimu inayoziwezesha Serikali mbali mbali Duniani kuimarisha dhana ya Demokrasia kupitia matangazo na taarifa za utekelezaji wa Ilani ya Chama tawala, miongozo na mipango ya maendeleo ili wananchi wajue uwajibikaji wa serikali yao na kupima uhalisia wa sera zinazotekelezwa kama zinakidhi mahitaji yao.
Maelezo hayo yametolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Bi. Catherine Peter Nao katika mwendelezo wa ziara yake katika vyombo Zanzibar, aliwaagiza viongozi na watendaji wa Chama na Serikali kupanga utaratibu wa   kuzungumza na vyombo vya Habari mara kwa mara  ili waweze kuwaeleza wananchi utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku katika taasisi zao.
Catherine alisema kiongozi yeyote mwenye dhamana ya kutoa taarifa za Chama ama Serikali atakayekataa kuzungumza na vyombo vya habari atakuwa anaenda kinyume na falsafa ya CCM mpya na Tanzania mpya inayotaka Chama kirudi mikononi mwa wananchi kwa kuanza na hatua ya kuwapatia taarifa sahihi zinazohusu masuala ya maendeleo.
Alisema kiongozi anayetekeleza wajibu wake vizuri hawezi kuwa na hofu ya kuzungumza na vyombo vya habari, hivyo ni lazima watumishi hao wa umma kukubali mabadiliko ya zama mpya za utandawazi zinazotoa fursa ya wananchi kuhoji na kudadisi viongozi waliowapa dhamana nini wamefakanya katika maeneo yao.
“Serikali ya Mapiunduzi ya Zanzibar chini ya uongozi wa Dk. Ali Mohamed Shein imefanya mambo mengi mazuri lakini cha kusikitisha wananchi wengi hawajui serikali yao nini inafanya kutokana na baadhi ya Viongozi wenye dhamana ya kuzungumza wapo kimya”, alisema Catherine.
 KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Ndugu Catherine Peter Nao akizungumza mara baada ya kuwasili katika studio za Chuchu FM iliyopo Mlandege Zanzibar.
 Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Ndugu Catherine Peter Nao akizungumza mara baada ya kuwasili katika studio za Swahiba Fm iliyopo Mbweni  Zanzibar.
 Mhariri wa Zanzibar leo Juma Khamis (aliyesimama akizungumza mwenye shati la mistari) akiwatambulisha wafanyakazi wa Shirika la Magazeti ya Serikali Zanzibar waliokuwepo katika Chumba cha Habari baada ya kutembelewa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Ndugu Catherine Peter Nao.
 Mkurugenzi wa Swahiba Fm, Maalim Kassim Mohamed Kassim(kulia) akizungumza na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Ndugu Catherine Peter Nao mara baada ya kuwasili katika Kituo cha radio hiyo kwa ajili ya kujitambulisha.
MKUU wa Waandishi wa habari Zanzibar leo Ndugu Mwantanga Ame (kulia) awakionyeshwa machapisho mbali mbali ya Gazeti la Zanzibar leo Toleo la No.5804 la Machi 1, 2018 Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Ndugu Catherine Peter Nao (kushoto) na Katibu msaidizi wa Idara hiyo Daud Ismail Juma(wa pili kushoto).


Hivyo makala CCM ZANZIBAR YATOA AGIZO ZITO KWA VIONGOZI WA CHAMA NA SERIKALI

yaani makala yote CCM ZANZIBAR YATOA AGIZO ZITO KWA VIONGOZI WA CHAMA NA SERIKALI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala CCM ZANZIBAR YATOA AGIZO ZITO KWA VIONGOZI WA CHAMA NA SERIKALI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/03/ccm-zanzibar-yatoa-agizo-zito-kwa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "CCM ZANZIBAR YATOA AGIZO ZITO KWA VIONGOZI WA CHAMA NA SERIKALI"

Post a Comment

Loading...