Loading...

CHAMWINO YAJIPANGA KUTOKOMEZA MIMBA ZA UTOTONI

Loading...
CHAMWINO YAJIPANGA KUTOKOMEZA MIMBA ZA UTOTONI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa CHAMWINO YAJIPANGA KUTOKOMEZA MIMBA ZA UTOTONI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : CHAMWINO YAJIPANGA KUTOKOMEZA MIMBA ZA UTOTONI
link : CHAMWINO YAJIPANGA KUTOKOMEZA MIMBA ZA UTOTONI

soma pia


CHAMWINO YAJIPANGA KUTOKOMEZA MIMBA ZA UTOTONI

Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma imejipanga kupambana na kutokomeza mimba za utotoni katika Wilaya hiyo.

Akizungumza katika uzinduzi wa Kapeni ya Kutokomeza Mimba za Utotoni katika Shule za Msingi na Sekondari katika Kata ya Haneti Wilayani Chamwino Diwani wa Kata ya Haneti Mhe. Peter Elia Chidawali amesema kuwa Kata yake na Wilaya kwa ujumla wamejipanga katika kupambana na vitendo vya ukatilia wa kijinsia yakiwemo matukio ya mimba na ndoa za utotoni .

Mhe. Peter Elia Chidawali ameongeza kuwa hawatakubali kuona watoto wao wanapoteza haki yao ya msingi ya kuendelezwa ya kupata Elimu kwa kupata mimba au kuolewa wakiwa bado shuleni.“Tutaendeleza Kampeni katika ngazi za familia kwa kuwaelimisha wazazi na walezi kuhusu madhara ya mimba za utotoni ili tuokoe kizazi cha kesho”alisema Mhe. Chidawali.

Naye Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Watoto kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi Rose Minja amesema kuwa suala la mimba za utotoni limezidi kuongeza siku hadi siku hivyo basi Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto alizindua Kampeni ya Kutokomeza Mimba za utotoni kwa lengo la kuwezesha utoaji wa elimu kwa wanafunzi, wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kushiriki mapambano dhidi tatizo hili.
Diwani wa Kata ya Haneti Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma Mhe. Peter Elia Chidawali akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi na Sekondari Haneti wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuzuia Mimba za Utotoni ijulikanayo ‘Mimi ni Msichana Najitambua Elimu ndio Mpango Mzima’ Wilayani Chamwino.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Watoto kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi Rose Minja akitambulisha Kampeni ya Kitaifa ya Kuzuia Mimba za Utotoni kwa wanafunzi wa shule sambamba na utekelezaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatil idhidi ya Wanawake na watoto katika Kata ya Haneti, wilayani Chamwino.
Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Bi. Shukuru Shanjala akiwaasa watoto wa kike kujitambua na kujilinda dhidi ya mimba za utotoni ili kupata haki ya kuendelezwa na kutoa mchango katika kufikia uchumi wa kati na maendeleo ya viwanda wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuzuia mimba za utotoni Kata ya Haneti, wilayani Chamwino.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi na Sekondari Haneti Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma wakisikiliza ushauri wa malezi na makuzi kutoka kwa wataalamu jinsia ili kuwawezesha kupambana na mimba za utotoni wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuzuia Mimba za Utotoni ijulikanayo Mimi ni Msichana Najitambua Elimu ndio Mpango Mzima Wilayani humo.



Hivyo makala CHAMWINO YAJIPANGA KUTOKOMEZA MIMBA ZA UTOTONI

yaani makala yote CHAMWINO YAJIPANGA KUTOKOMEZA MIMBA ZA UTOTONI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala CHAMWINO YAJIPANGA KUTOKOMEZA MIMBA ZA UTOTONI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/03/chamwino-yajipanga-kutokomeza-mimba-za.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "CHAMWINO YAJIPANGA KUTOKOMEZA MIMBA ZA UTOTONI"

Post a Comment

Loading...