Loading...
title : DC WA KIBAHA ASSUMPTER MSHAMA AAHIDI NEEMA KWA KINAMAMA WILAYANI HUMO
link : DC WA KIBAHA ASSUMPTER MSHAMA AAHIDI NEEMA KWA KINAMAMA WILAYANI HUMO
DC WA KIBAHA ASSUMPTER MSHAMA AAHIDI NEEMA KWA KINAMAMA WILAYANI HUMO

MKUU wa Wilaya ya Kibaha Bi Assumpter Mshama amewaahidi kina mama wajasiriamali wa Wilaya ya Kibaha kuwa atazungumza na uongozi wa Halmashauri ya Mji ili itengwe siku na eneo maalum kwa ajili ya kufanya maonyesho ya bidhaa wanazozitengeneza ikiwa ni katika kupambana na changamoto ya ukosefu wa masoko ya kuuzia bidhaa hizo.
Mshama amesema hayo alipokuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani Kibaha Mkoa wa Pwani, amewataka wanawake kujiamini, kushikamana na kuachana na dhana potofu ya kupigana vita katika maeneo mbalimbali kwani adui wa mwanamke ni mwanamke mwenyewe.
Aidha amesema kutokana na wanawake wengi kutofahamu sheria za ndoa na mirathi , talaka na sheria ya ardhi ya mwaka 1999, Halmashauri ya Kibaha itaendelea kutoka elimu ya sheria kwa kupitia wadau wa masuala ya sheria.
Amewataka wanawake wote nchini kuitafakari siku hii maalum kwa kutafakari mafanikio na changamoto na kuweka utatuzi wa changamoto wanazokabiliana nazo wanawake huku kauli mbiu ikisema kuelekea uchumi wa viwanda tuimarishe uswa wa jinsia na uwezeshaji wanawake vijijini kauli mbiu hii inahamasisha jamii kuongeza fursa za kiuchumi kwa wanawake ili kuwajengea uwezo katika nyanja zote za maendeleo, kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni na kitaaluma.
Hivyo makala DC WA KIBAHA ASSUMPTER MSHAMA AAHIDI NEEMA KWA KINAMAMA WILAYANI HUMO
yaani makala yote DC WA KIBAHA ASSUMPTER MSHAMA AAHIDI NEEMA KWA KINAMAMA WILAYANI HUMO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC WA KIBAHA ASSUMPTER MSHAMA AAHIDI NEEMA KWA KINAMAMA WILAYANI HUMO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/03/dc-wa-kibaha-assumpter-mshama-aahidi.html
0 Response to "DC WA KIBAHA ASSUMPTER MSHAMA AAHIDI NEEMA KWA KINAMAMA WILAYANI HUMO"
Post a Comment