Loading...

DED Kishapu asisitiza uwajibika kwa walimu

Loading...
DED Kishapu asisitiza uwajibika kwa walimu - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DED Kishapu asisitiza uwajibika kwa walimu, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DED Kishapu asisitiza uwajibika kwa walimu
link : DED Kishapu asisitiza uwajibika kwa walimu

soma pia


DED Kishapu asisitiza uwajibika kwa walimu

Na Robert Hokororo, Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga amesisitiza uwajibikaji kwa walimu ili kuleta ufanisi mkubwa katika sekta ya elimu.
Magoiga alitoa msisitizo huo wakati akikabidhi vyumba viwili vya madarasa kwa shule ya sekondari Maganzo wilayani humo vilivyokamilika vyenye thamani ya sh. milioni 19.4.
Vyumba hivyo ni sehemu ya mradi uliotekelezwa na Halmashauri ya wilaya hiyo kutokana na fedha ambazo zilitolewa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).
Alisema kuwa endapo walimu hao watawajibika ipasavyo wanafunzi watafanya vizuri katika masomo yao na hivyo kuleta sifa nzuri katika shule pamoja na wilaya nzima kwa ujumla.
Mkurugenzi Mtendaji aliongeza kwa kusema kuwa kampeni ya kufuta ziro yaani sifuri inayoendelea itaweza kupata mafanikio makubwa kama walimu watajituma katika kufundisha vizuri.
Aidha aliwataka wanafunzi kujituma na kutumia fursa ya kuwepo shuleni kwa ajili ya kusoma kwa bidii na kufaulu masomo yao hivyo kuweza kuwa watalaamu wa baadaye kwa manufaa ya jamii.
Itakumbukwa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2017/2018 Halmashauri ilipata ufadhili wa fedha TEA jumla ya sh. milioni 70.5 kati y ash. milioni 141 kwa ajili ya ujenzi wa ujenzi wa miundombinu katika shule hiyo.
Kwa kutumia fedha hizo pamoja na kushirikisha nguvu za wananchi inaendelea na ujenzi wa nyumba ya walimu sita, choo cha matundu 2 cha walimu.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga (mwenye tai) akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Maganzo wakati alipozindua vyumba vya madarasa vilivyokamilika.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga akifungua moja ya vyumba vya madarasa vilivyomalika ujenzi wake wakati akivikabidhi kwenye shule ya sekondari Maganzo.
 Walimu, wajumbe wa bodi ya shule na wanafunzi (hawapo pichani) wa shule ya sekondari  Maganzo wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga (aliyesimama) wakati alipozungumza alipowakabidhi vyumba vya madarasa.
 Sehemu ya jengo lenye chumba cha darasa la shule ya sekondari Maganzo lililokamilika ujenzi wake na kukabidhiwa.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala DED Kishapu asisitiza uwajibika kwa walimu

yaani makala yote DED Kishapu asisitiza uwajibika kwa walimu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DED Kishapu asisitiza uwajibika kwa walimu mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/03/ded-kishapu-asisitiza-uwajibika-kwa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "DED Kishapu asisitiza uwajibika kwa walimu"

Post a Comment

Loading...