Loading...
title : DKT KIJAJI AZINDUA MKTABA WA HUDUMA KWA WATEJA WA CMSA
link : DKT KIJAJI AZINDUA MKTABA WA HUDUMA KWA WATEJA WA CMSA
DKT KIJAJI AZINDUA MKTABA WA HUDUMA KWA WATEJA WA CMSA
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk.Ashanti Kijaji amesema kuwa mamlaka ya Masoko na Mitaji ni injini katika maendeleo ya uchumi hivyo ni lazima mamlaka hiyo iwafikie wateja.
Kijaji aliyasema hayo wakati akitunuku vyeti kwa wahitimu wa mamlaka hiyo waliopata kwa kushirikiana na chuo cha Uingereza CISI katika fani ya masoko na mitaji, amesema kuwa watu hawana uelewa juu ya masoko na mitaji hivyo wanatakiwa kufikia wateja katika kutimiza adhima ya serikali ya awamu ya tano yenye Kauli mbiu ya nchi ya viwanda.
Amesema Mamlaka kwa kutumia watalaam hao lazima wafanye kazi katika kujenga nchi na kutoa elimu kuhusiana na masoko na mitaji.Amesema kuwa kampuni zipo nyingi lakini hazijaweza kuingia katika soko la hisa ni kutokana na kampuni hizo kushindwa kufikiwa ikiwa ni pamoja na kupata elimu.
Naibu Waziri huyo amesema kuwa katika kufanya kazi mamlaka hiyo lazima iweke mpango mkakati katika kuhamasisha kampuni ziingie katika soko la hisa.Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka hiyo,Dk.John Mduma amesema kuwa wanaendelea katika kutoa huduma ikiwa ni pamoja kufanyia kazi maagizo ya Naibu Waziri katika kuwafikia wateja na kuleta matokeo chaya ya maendeleo ya uchumi.
Dk. Mduma amesema kuwa katika kuwa sasa watafungua dirisha la uhamasishaji katika kufikia kampuni ziweze kuingia katika soko la hisa.
Afisa Mtendaji Mkuu , Nicodemus Mkama amesema mkataba wa huduma kwa wateja waliouzindua watawafikia wateja wote kuingia dhamana ya masoko na mitaji katika kuendrleza miradi mbalimbali nchini.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa CMSA, Nicodemus Mkama akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi katika uzinduzi w akitabu cha huduma kwa wateja.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashantu Kijaji, akizindua kitabu cha Msaada wa huduma kwa wateja
Mwenyekiti wa TSEBA,George Fumbuka akitoa neno la Shukrani kwa waziri mara baada ya kumaliza kuzinduliwa kwa kitabu cha Mkataba wa huduma kwa wateja.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashantu Kijaji, akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa wahitimu wa kozi ya ushiriki katika Masoko
Baadhi ya Wadau walioshiriki katika uzinduzi wa kitabu cha huduma kwa wateja
Hivyo makala DKT KIJAJI AZINDUA MKTABA WA HUDUMA KWA WATEJA WA CMSA
yaani makala yote DKT KIJAJI AZINDUA MKTABA WA HUDUMA KWA WATEJA WA CMSA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DKT KIJAJI AZINDUA MKTABA WA HUDUMA KWA WATEJA WA CMSA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/03/dkt-kijaji-azindua-mktaba-wa-huduma-kwa.html
0 Response to "DKT KIJAJI AZINDUA MKTABA WA HUDUMA KWA WATEJA WA CMSA"
Post a Comment