Loading...
title : KESI YA ALIYEKUWA MHASIBU WA TAKUKURU KUANZA KUSIKILIZWA APRILI 10
link : KESI YA ALIYEKUWA MHASIBU WA TAKUKURU KUANZA KUSIKILIZWA APRILI 10
KESI YA ALIYEKUWA MHASIBU WA TAKUKURU KUANZA KUSIKILIZWA APRILI 10
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii
Kesi dhidi ya Mhasibu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Godfrey Gugai anayedaiwa kuwa na utajiri wa kutisha kwa kumiliki mali zenye thamani ya Sh. 3 bilioni ambazo haziendani na kipato chake kuanza kusikilizwa mapema mwezi ujao.
Hayo yameelezwa leo Machi 20, 2018 na wakili wa serikali kutoka Takukuru, Vitalis Peter mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.
"Mheshimiwa kesi hii leo ilikuja kwa ajili ya kutajwa lakini upelelezi umekamilika, tunaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kuja kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali (PH).
Kufuatia taarifa hiyo, hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Aprili 10, mwaka huu. Kwa ajili ya washtakiwa kusomewa Maelezo ya awali.
Mbali na Gugai, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni George Makaranga, Leonard Aloys na Yasini Katera
Washtakiwa hao wanaokabiliwa na mashtaka 43 yakiwemo 20 ya utakatishaji fedha haramu, kumiliki mali zisizoendana na kipato na kughushi mikataba ya mauziano ya viwanja katika maeneo mbalimbali.
Gugai na wenzake wanasota mahabusu kutokana na kukabiliwa na mashtaka ya utakatishaji fedha ambayo hayana dhamana kwa mujibu wa sheria.
Hivyo makala KESI YA ALIYEKUWA MHASIBU WA TAKUKURU KUANZA KUSIKILIZWA APRILI 10
yaani makala yote KESI YA ALIYEKUWA MHASIBU WA TAKUKURU KUANZA KUSIKILIZWA APRILI 10 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KESI YA ALIYEKUWA MHASIBU WA TAKUKURU KUANZA KUSIKILIZWA APRILI 10 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/03/kesi-ya-aliyekuwa-mhasibu-wa-takukuru.html
0 Response to "KESI YA ALIYEKUWA MHASIBU WA TAKUKURU KUANZA KUSIKILIZWA APRILI 10"
Post a Comment