Loading...
title : MAKAMU WA RAIS AWEKA SHADA LA MAUA KWENYE LA Dkt. OMAR ALI JUMA
link : MAKAMU WA RAIS AWEKA SHADA LA MAUA KWENYE LA Dkt. OMAR ALI JUMA
MAKAMU WA RAIS AWEKA SHADA LA MAUA KWENYE LA Dkt. OMAR ALI JUMA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo ameanza ziara ya siku tatu Pemba ikiwa na lengo la kuhamasisha shughuli za maendeleo.
Makamu wa Rais ambaye amewasili Pemba alasiri ya leo na kupokelewa na viongozi mbali mbali wa Serikali na Chama ambapo alipokea taarifa za mikoa miwili ya Pemba. Pia Makamu wa Rais alizuru kaburi la Dkt. Omar Ali Juma lililopo Wawi, Pemba na kuweka shada la maua.
Aidha Makamu wa Rais aliwataka Wananchi wa Chumbageni kukumbuka historia na kurudi nyumbani, Makamu wa Rais aliyasema hayo mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Tawi la CCM Chumbageni Wambaa.
Kesho Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan anatazamiwa kuendelea na ziara yake ambapo ataweka jiwe la msingi katika Kituo cha Huduma za Mama na Mtoto Shumba Vyamboni .
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikabidhiwa shada la maua kwenye kaburi la Marehemu Dkt. Omar Ali Juma lililopo Wawi,Pemba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka shada la maua kwenye kaburi la Marehemu Dkt. Omar Ali Juma lililopo Wawi,Pemba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)Dk Omar Ali Juma (26 Juni 1941 – 4 Julai 2001) alikuwa Makamu wa Rais wa Serikali ya Awamu ya Tatu nchini Tanzania, iliyokuwa inaongozwa na Rais Benjamin William Mkapa
Hivyo makala MAKAMU WA RAIS AWEKA SHADA LA MAUA KWENYE LA Dkt. OMAR ALI JUMA
yaani makala yote MAKAMU WA RAIS AWEKA SHADA LA MAUA KWENYE LA Dkt. OMAR ALI JUMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAKAMU WA RAIS AWEKA SHADA LA MAUA KWENYE LA Dkt. OMAR ALI JUMA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/03/makamu-wa-rais-aweka-shada-la-maua.html
0 Response to "MAKAMU WA RAIS AWEKA SHADA LA MAUA KWENYE LA Dkt. OMAR ALI JUMA"
Post a Comment