Loading...
title : MAKAMU WA RAIS AZUNGUMZIA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI
link : MAKAMU WA RAIS AZUNGUMZIA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI
MAKAMU WA RAIS AZUNGUMZIA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI
Kauli Mbiu: Kuelekea Uchumi wa Viwanda tuimarishe usawa wa kijinsia na Uwezeshaji wa Wanawake Vijijini.
Leo katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, Mimi kama mwanamke na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nina kila sababu ya kuzungumza japo kwa kifupi jitihada mbalimbali zilizochukuliwa na zinazoendelea kuchukuliwa na serikali katika kuimarisha usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wa Wanawake Vijijini.
· Serikali inayo Sera ya kuendeleza Wanawake, Sheria za ardhi za mwaka 1999 ambazo husimamia haki za wanawake katika kumiliki ardhi.
· Sera ya elimu bure inayotekelezwa na serikali ya awamu ya tano imetoa fursa kwa watoto wengi wa kike kuandikishwa shuleni.
· Kuboreshwa kwa huduma za kijamii kama vile kujengwa zahanati na vituo vya afya na usambazaji wa maji vimempunguzia mwanamke usumbufu na hivyo kumpa muda wa kutosha kufanya shughuli za maendeleo.
· Usambazaji umeme vijijini kwa kiasi kikubwa umesaidia wanawake wengi kujishughulisha na shughuli mbalimbali za kujiingizia kipato.
· Uwezeshaji wa Wanawake kwa kuwapatia asilimia 5 ya mapato ya halmashauri na asilimia 30 ya zabuni za halmashauri kumewawezesha wanawake wengi kufanya biashara na hatimaye kuwa na uhakika wa kipato .
· Serikali kuendelea kuhimiza taasisi za kifedha kutoa mikopo yenye riba nafuu ili kuwawezesha wanawake wengi kunufaika na mikopo hiyo.
· Kurasimisha vikoba pamoja na kuwashawishi wanawake wengi zaidi kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii ili kuweza kunufaika na mafao na mikopo itolewayo na taasisi hizo.
Hivyo makala MAKAMU WA RAIS AZUNGUMZIA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI
yaani makala yote MAKAMU WA RAIS AZUNGUMZIA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAKAMU WA RAIS AZUNGUMZIA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/03/makamu-wa-rais-azungumzia-siku-ya.html
0 Response to "MAKAMU WA RAIS AZUNGUMZIA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI"
Post a Comment