Loading...

MAKONDA AFANIKISHA SAFARI YA MATIBABU YA ALBAITY CHINA

Loading...
MAKONDA AFANIKISHA SAFARI YA MATIBABU YA ALBAITY CHINA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAKONDA AFANIKISHA SAFARI YA MATIBABU YA ALBAITY CHINA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAKONDA AFANIKISHA SAFARI YA MATIBABU YA ALBAITY CHINA
link : MAKONDA AFANIKISHA SAFARI YA MATIBABU YA ALBAITY CHINA

soma pia


MAKONDA AFANIKISHA SAFARI YA MATIBABU YA ALBAITY CHINA

Na Emmanuel Masaka, Globu ya Jamii

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amekabidhi tiketi za ndege za watu wanne kwa ajili ya safari ya matibabu ya kijana Ahmed Albaity ambaye ambaye anakwenda kutibiwa nchini China kwenye Hospitali ya Beijing.

Albaity amekuwa akiteseka kwa zaidi ya miaka 10 akiwa kitandani kutokana na kushindwa kumudu gharama za matibabu lakini leo hii Makonda amefanikisha ndoto yake ya kumkabidhi tiketi kwa ajili kwenda nchi humo akatibiwe.
Makonda mbali ya kukabidhi tiketi, pia amejitolea kugharamia fedha za matibabu na malazi na alitoa ahadi ya kumsaidia Albaity wakati wa mchakato wa upimaji afya bure kwenye meli ya Jeshi la China mwishoni mwa mwaka jana baada ya kugundulika kijana huyo anahitaji matibabu maalumu ambayo yanapatikana katika nchi ya China tu.

Hali hiyo ilimfanya Makonda kutokwa na machozi na kuahidi kumpeleka China akatibiwe kwa gharama yoyote ili maumivu na mateso anayoyapata yafike mwisho.Albaity anasumbuliwa na tatizo la uti wa mgongo baada ya kuanguka na kuvunjika shingo alipokuwa akiogelea ambapo kwa sindano moja pekee inagharimu dola za Marekani 26,000 sawa na Sh.milioni 52.

Akizungumza leo baada ya kukabidhi tiketi hizo,Makonda amesema Albaity atasafiri nchini China siku ya Jumapili akiongozana na watu wengine watatu wa kumsaidia ambapo gharama zake ni zaidi ya Sh.milioni 100.Makonda amesema shauku yake ni kugusa maisha ya kila mwananchi hata kama ni mmoja atakaekwenda mbele za Mungu na kusema ahsante Mungu kwa kutupatia viongozi wetu na kuongeza "Ifike mahali tumtumikie Mungu katika nafasi zetu.
"Na katika hilo watu wote watakuwa sawa na tutawahudumia bila kutarajia chochote kutoka kwao na tunachokifanya ni sehemu ya utumishi wetu.Niwashukuru wote waliochangia kwa ajili ya kusaidia kufanikisha matibabu haya,"amesema Makonda.

Ametoa mwito kwa wananchi wa dini zote kumuombea Albaity ili apone na kuendelea na shughuli za ujenzi wa Taifa.Kwa upande wa Albaity amemshukuru RC Makonda kwa moyo wa ukarimu aliouonyesha ambapo ameeleza ameishi kwa mateso muda mrefu kutokana na kukosa uwezo wa kumudu gharama za matibabu. 

"Wakati naomba watu wanichangie wapo watu waliokuwa wananivunja moyo kwa kuniambia siwezi kupona lakini Makonda ameonesha moyo wa kipekee,"amesema.


Hivyo makala MAKONDA AFANIKISHA SAFARI YA MATIBABU YA ALBAITY CHINA

yaani makala yote MAKONDA AFANIKISHA SAFARI YA MATIBABU YA ALBAITY CHINA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAKONDA AFANIKISHA SAFARI YA MATIBABU YA ALBAITY CHINA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/03/makonda-afanikisha-safari-ya-matibabu.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MAKONDA AFANIKISHA SAFARI YA MATIBABU YA ALBAITY CHINA"

Post a Comment

Loading...