Loading...

MAMA MWANAMEMA SHEIN AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI ZANZIBAR

Loading...
MAMA MWANAMEMA SHEIN AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI ZANZIBAR - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAMA MWANAMEMA SHEIN AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI ZANZIBAR, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAMA MWANAMEMA SHEIN AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI ZANZIBAR
link : MAMA MWANAMEMA SHEIN AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI ZANZIBAR

soma pia


MAMA MWANAMEMA SHEIN AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI ZANZIBAR

Akizungumza katika maadhimisho ya ‘Siku ya Wanawake Duniani’ yaliyofanyika leo Machi 8, 2018 katika kijiji cha Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja, mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, amesema wanawake ni nguzo muhimu ya kuinua familia  na wana mchango mkubwa katika kutekeleza majukumu ili kuziimarisha familia zao.
Mama Shein amesema akinamama wana mchango mkubwa katika kuimarisha familia ili zipate ustawi na kuzifanya zipige hatua zaidi ya maendeleo nchini, na kwamba wanawake na watoto ndio waathirika wakubwa kila kunapotokea matatizo nchini yenye mwelekeo wa kupoteza amani.
Kwa hivyo amesisitiza haja ya kuendeleza ushirikiano katika kuendeleza amani na mshikamano ili kuhakikisha wanawake na watoto wanakuwa salama na kuishi bila khofu. Aidha, Mama Shein aliwataka akinamama na akinababa kushirikiana katika malezi bora ya watoto kulingana na maadili, silka na utamaduni wa nchi ili wawe raia wema.
Kuhusu vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia vinavyoendelea kushamiri kwa kasi, Mama Mwanamwema alisema Zanzibar bila ya uovu huo unaoathiri maendeleo ya taifa inawezekana iwapo jamii itakuwa kitu kimoja kwa kushirikiana kuvikomesha
Sambamba na hayo, alisema katika kupinga mapambano dhidi ya maradhi ya ukimwi, wanawake wana mchango mkubwa wa kudhibiti maambukizo ya virusi ifikapo mwaka 2030.
Lakini alieleza kusikitishwa kwake na kiwango kikubwa cha wanawake wanaoambukizwa maradhi hayo ambako kiko juu kuliko kwa wanaume.
“Takwimu zinaonesha kuwa idadi ya wanawake wanaoishi na virusi vya ukimwi nchini ni mara mbili ya wanaume, hivyo tuchukuwe hatua madhubuti za kujiepusha na vitendo vinavyochangia kupata maradhi hayo,” alisisitiza.
Aidha aliwataka wanawake kuzitumia fursa za kujiunga na vikundi vya ushirika ili kujiimarisha kiuchumi kwa kujiongezea kipato na kupambana na umasikini, hali itakayoipa nguvu Serikali na washirika wengine kutanua wigo wa misaada yao.
 WAZIRI wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Zanzibar, Mhe. Maudline Cyrus Castico, akizungumza wakati wa hafla ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani iliofanyika katika viwanja vya Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja, kabla ya kumkaribisha mgeni rasmin Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein.
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiwahutubia Wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja wakati wa hafla ya maadhimisho Siku ya Wanawake Duniani,huadhimishwa kila mwaka ifikapo March 8, maadhimisho hayo yamefanyika katika viwanja vya Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja.( Picha na Yussuf Simai-Maelezo Zanzibar)


Hivyo makala MAMA MWANAMEMA SHEIN AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI ZANZIBAR

yaani makala yote MAMA MWANAMEMA SHEIN AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI ZANZIBAR Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAMA MWANAMEMA SHEIN AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI ZANZIBAR mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/03/mama-mwanamema-shein-aongoza.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MAMA MWANAMEMA SHEIN AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI ZANZIBAR"

Post a Comment

Loading...