Loading...
title : MEYA JIJI LA DAR AZIKUMBUSHA HALMASHAURI KUAJIRI WATUMISHI WA KUZIKA WASIOKUWA NA NDUGU
link : MEYA JIJI LA DAR AZIKUMBUSHA HALMASHAURI KUAJIRI WATUMISHI WA KUZIKA WASIOKUWA NA NDUGU
MEYA JIJI LA DAR AZIKUMBUSHA HALMASHAURI KUAJIRI WATUMISHI WA KUZIKA WASIOKUWA NA NDUGU
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
MEYA wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amezitaka halmashauri zote katika jiji hilp kuajiri watumishi ambao watakuwa wanazika miili ya watu ambao watabainika kutokuwa na ndugu wa kuwazika.
Ametoa kauli hiyo leo kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani wa Jiji la Dar es Salaam ,ambapo amewaambia madiwani hao kuna taarifa amezipata za halmashauri kutokuajiri watumishi kwa akili ya kuzika watu wasiokuwa na ndugu.
Mwita amesema kuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam pamoja na halmashauri nyingine zilizopo jijini humo walikubaliana kuzika watu wasiokuwa na ndugu Dar."Hivyo marehemu wanapokuwa wamekaa muda mrefu wanalazimika kuzika na Jijijiji,na tulikubali kuchangia usafiri,dawa na sanda," amesema.
Amefafanua kuwa watu hao wasiokuwa na ndugu wanapokufa wapo ambao wanakaa hospitalini zaidi ya siku 20,hivyo wapo ambao wanazika kwenye halmashauri mbalimbali.Hivyo wakati Jiji la Dar es Salaam likitimiza wajibu katika kupumzisha mwili wa marehemu,halmashauro jukumu lao ni kutoa watumishi kwa ajili ya kuzika.
Amefafanua taarifa alizonazo ni Halmashauri ya Kinondoni pekee ndio ambayo imeajiri watumishi kwa ajili ua kuzika miili ya watu ambao wamefariko na hawana ndugu.Hivyo amezikumbusha halmashauri zote kuajiri watumishi hao ili kufanikisha kupumzisha miili hiyo.
"Ni wajibu wa halmashauri kuhakikisha wanafanikisha kupatikana kwa watumishi hao haraka," amesema Meya Mwita.
Hivyo makala MEYA JIJI LA DAR AZIKUMBUSHA HALMASHAURI KUAJIRI WATUMISHI WA KUZIKA WASIOKUWA NA NDUGU
yaani makala yote MEYA JIJI LA DAR AZIKUMBUSHA HALMASHAURI KUAJIRI WATUMISHI WA KUZIKA WASIOKUWA NA NDUGU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MEYA JIJI LA DAR AZIKUMBUSHA HALMASHAURI KUAJIRI WATUMISHI WA KUZIKA WASIOKUWA NA NDUGU mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/03/meya-jiji-la-dar-azikumbusha.html
0 Response to "MEYA JIJI LA DAR AZIKUMBUSHA HALMASHAURI KUAJIRI WATUMISHI WA KUZIKA WASIOKUWA NA NDUGU"
Post a Comment