Loading...
title : Mfumo wa kujitegemea wa usajili wa vizazi kwa watoto wa chini ya umri miaka mitano umeanzishwa katika Mikoa ya Mara na Simiyu
link : Mfumo wa kujitegemea wa usajili wa vizazi kwa watoto wa chini ya umri miaka mitano umeanzishwa katika Mikoa ya Mara na Simiyu
Mfumo wa kujitegemea wa usajili wa vizazi kwa watoto wa chini ya umri miaka mitano umeanzishwa katika Mikoa ya Mara na Simiyu
Waziri wa Haki na Katiba, Prof Palamaganda Kabudi akionesha kitabu cha vyeti vya kuzaliwa pamoja na simu ya kisasa alipozindua zoezi la usajili na utoaji vyeti vya kuzaliwa kwa njia ya mtandao kwa mikoa ya Mara na Simiyu. Tigo imetoa simu 1125 za thamani ya Tsh 77milioni kufanikisha zoezi hill. Kulia ni Mwenyekiti was Bodi ya RITA, Prof. Hamisi Dihenga.
MARA – Mkoa wa Mara na Simiyu imezindua kuanza kwa mfumo wa kujitegemea wa usajili wa vizazi ambao unatarajiwa kunufaisha zaidi ya watoto 700,000 walioko chini ya umri wa miaka mitano katika mikoa hiyo.
Uzinduzi huo uliofanyika katika mji wa Musoma, ulihudhuriwa na Mheshimiwa Waziwa wa Katiba na Kisheria Profesa Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi, UNICEF na Mwakilishi wa Serikali ya Canada na wageni wengine mashuhuri. Mfumo huo wa usajili uliorahisishwa utasaidia usajili wa watoto wote wachanga na kupunguza idadi kubwa ya watoto ambao hawajasajiliwa walioko chini ya umri wa miaka mitano katika mikoa hiyo miwili.
Mfumo huu ambao unajitegemea usio ratibiwa kutoka serikali kuu unasogeza huduma ya usajili karibu na jamii. Inaanzisha vituo vya usajili katika vituo vya afya, ambavyo vinatoa huduma ya afya ya uzazi na watoto, na kwenye jamii katika ofisi za mtendaji wa kata kuendana na sera ya serikali ya ugawaji wa madaraka kwa serikali mitaa.
Zoezi hili limeziba pengo la mijini na vijijini, kwa kuzipa jamii za pembezoni nafasi ya kusajili watoto wao. Inatatua suala la msingi la upatikanaji na uwezo wa kumudu jambo ambalo limekuwa ni kikwazo kikubwa katika usajili wa vizazi nchini Tanzania.
Hivyo makala Mfumo wa kujitegemea wa usajili wa vizazi kwa watoto wa chini ya umri miaka mitano umeanzishwa katika Mikoa ya Mara na Simiyu
yaani makala yote Mfumo wa kujitegemea wa usajili wa vizazi kwa watoto wa chini ya umri miaka mitano umeanzishwa katika Mikoa ya Mara na Simiyu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mfumo wa kujitegemea wa usajili wa vizazi kwa watoto wa chini ya umri miaka mitano umeanzishwa katika Mikoa ya Mara na Simiyu mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/03/mfumo-wa-kujitegemea-wa-usajili-wa.html
0 Response to "Mfumo wa kujitegemea wa usajili wa vizazi kwa watoto wa chini ya umri miaka mitano umeanzishwa katika Mikoa ya Mara na Simiyu"
Post a Comment